Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Angellah Kairuki, ameshiriki katika Kongamano la Uchaguzi, Amani na Dua lililoandaliwa na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Ubungo, Jimbo la Kibamba. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mhe. Kairuki amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani, huku akisisitiza umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka kwa hiari na utulivu.
Aidha, amewaomba masheikh na viongozi wa dini kuendelea kuhimiza amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania kipindi chote cha uchaguzi.
Mhe. Kairuki pia amewasihi waumini wa Kiislam wa Jimbo la Kibamba pamoja na Watanzania kwa ujumla kumpigia kura za ndiyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumpa kura nyingi yeye kama Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba, pamoja na madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...