BARAZA La Sanaa (BASATA) lafungua rasmi dirisha la Kupendekeza Kazi za Wasanii katika tuzo za Muziki nchini TMA zinazotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu.
Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 24,2025 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana amesema dirisha la Kupendekeza kazi za Sanaa tayari limefunguliwa hivyo Wasanii wachangamkie fursa hiyo.
"Msimu wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2024) umeanza rasmi leo, huku mfumo wa kupokea kazi za wasanii kwa ajili ya kushindanishwa katika vipengele mbalimbali ukianza kufanya kazi rasmi.
Hata hivyo Mapana ameeleza kuwa Katika Tuzo hizo zitashindaniwa katika vipengele 36 ambapo Wasanii watakaopendekeza kazi zao Wanatakiwa Kuwa na Usajili katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili waweze kukidhi viwango vya kuweza kushiriki katika kinyang'anyiro hicho.
Pia ameongeza kuwa tuzo hizo zitafanyika Disemba 13,2025 Jijini Dar es Salaam huku Kilele cha Mapendekezo ya kazi hizi na uwasilishaji mwisho wake utakuwa mwezi Novemba mwaka huu na Kuongeza kuwa lengo kuu la tuzo hizo ni kutambua, kuthamini na kuenzi mchango wa wasanii wa muziki nchini Tanzania, pamoja na kuhamasisha ubunifu, umahiri na ushindani chanya katika tasnia ya muziki.
“Tunatoa jukwaa la kipekee la kuonyesha ubunifu, ujuzi na mafanikio ya wasanii wetu katika kukuza utamaduni, burudani na uchumi wa sanaa,”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...