Songea,Ruvuma.
Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Kata ya Mjini zimehitimishwa rasmi Oktoba 26 2025, kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Mashujaa Tawi la Mashujaa, uliovutia wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Katika kufunga kampeni hizo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliongozwa na mgombea wake wa nafasi ya Udiwani Mathew Ngalimanayo, ambaye amesisitiza dhamira ya chama hicho kuendeleza kasi ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii katika kata hiyo.
Akitoa tathmini ya hali ya maendeleo, Ngalimanayo alibainisha kuwa changamoto iliyosalia inayowakabili wakazi wa Kata ya Mjini ni miundombinu ya barabara, ameweka wazi mpango wa kujenga barabara zenye jumla ya urefu wa kilomita 10.1, zitakazojumuisha maeneo ya Mjini, Mfaranyaki na Majengo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Barabara ya SOUWASA–Mashujaa kuelekea Mahenge imepewa kipaumbele maalum na inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ili kurahisisha usafiri na kukuza shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Mbali na miundombinu, Ngalimanayo ameeleza kuwa serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wa wananchi kwa kutoa mikopo kupitia vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, hatua hiyo inalenga kuongeza ajira, kukuza kipato na kuinua uchumi wa kata hiyo.
Ameeleza kuwa CCM itaendelea kuwa nguzo ya amani na umoja wa taifa, huku akisisitizwa kuwa ni chama pekee chenye uzoefu na uwezo wa kusimamia maendeleo bila migogoro wala vurugu.
Katika kuelekea siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wananchi wa Kata ya Mjini wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo, wakichagua viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Mbunge hadi Diwani, ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Ngalimanayo ameahidi kutumia nafasi yake ndani ya Baraza la Madiwani kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, kuhakikisha rasilimali za kata zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote.
Wakati huo huo, baadhi ya watia nia ya kugombea nafasi hiyo wameamua kumuunga mkono Ngalimanayo, wakitambua mchango na ufanisi wa CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kampeni hizo zimefungwa kwa amani na mshikamano mkubwa, huku wananchi wakionesha matumaini makubwa ya kuendelea kushuhudia mageuzi ya maendeleo katika Kata ya Mjini chini ya uongozi wa CCM.

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...