Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Geita

MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema mkakati wa Serikali katika miaka mitano ijayo itaweka nguvu katika ng’ombe wa maziwa lengo likiwa kuinyanyua sekta ya maziwa ili wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wanufaike na kuinua vipato vyao.

Akizungumza leo Oktoba 11,2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Shule ya Msingi Bukombe mkoani Geita Dk.Samia ambaye anaendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura kuelekea Oktoba 29, amesema Wilaya ya Bukombe inawafugaji wa kawaida wa ng’ombe wa nyama lakini na ng’ombe wa maziwa.

“Tunachojipanga Serikali yenu wana Bukombe mbali na kuongeza nguvu kwenye sekta ya mifugo kwa ujumla kwa kutoa ruzuku ya chanjo, kujenga majosho,kukarabati minada na kujenga minada mipya pamoja na kujenga machinjio…

“Tumeanua  sasa tuingie kwenye ng’ombe wa maziwa ,tuinyanyue sekta ya maziwa na Bukombe ni wazalishaji wazuri wa maziwa.Tunakwenda kunyanyua sekta ya maziwa,pia kuweke viwanda vitakavyochakata maziwa ili maziwa yawe bidhaa na wafugaji wauze bidbaa hiyo wapate fedha ziingie mfukoni na maisha yaendelee hiyo ndio kazi na utu.”

Aidha Mgombea Dk.Samia Suluhu Hassan amesema pia Bukombe ni ya wakulima wa mahindi,mpunga,viazi na mazao mengine wakulima wa Bukombe kwa muda mrefu walikuwa wanataka walime wavune kwa kiasi kikubwa na wafanyebiashara wapate fedha wajisaidie .

“Tulichokifanya Serikali ni kuwaletea ruzuku ya mbolea,ruzuku ya dawa za kilimo, lakini kuwajengea skimu za umwagiliaji maji ili wakulima wazalishe kwa wingi kisha wauze wapete fedha za kuendesha maisha yao.Hivyo ndivyo serikali hii tunavyowalea wakulima.”




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...