*Akinamama wanaokwenda kujifungua hospitali ya Mawenzi sasa imefikia 328,502
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kilimanjaro
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan
amesema Serikali katika mitano iliyopita imefanya maboresho makubwa katika sekta ya afya mkoani Kilimanjaro ikiweko maboresho makubwa katika hospitali ya Mawenzi.
Amesema kwamba kutokana na maboresho yaliyofanywa na serikali katika afya imewezesha pia kinamama wanaoitika kwenda hospitali imeongeza kutoka 260,486 hadi 328,502 mwaka huku kwa kiasi kikubwa serikali imepunguza vifo vya kinamama wakati wa kujifungua na hizo jitihada zitaendelea.
Akizungumza leo Oktoba 1,2025 katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro mbele ya maelfu ya wananchi wa mkoa huo pamoja na mambo mengine Dk.Samia amesema katika Hospitali ya Mawenzi Serikali imefanya maboresho makubwa katika hospotali hiyo
“Serikali imefanya maboresho makubwa katika hospitali ya Mawenzi ambapo nilikuja kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la kinamama na watoto. Jengo hilo limeshakamilika na limeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Amesema kuwa uwepo wa jengo hilo limewezesha kinamama kuongezeka kupata huduma ya kujifungua katika hospitali.
"Kinamama wanaoitika kwenda hospitali imeongeza kutoka 260,486 hadi 328,502.Kwa kiasi kikubwa tumepunguza vifo vya kinamama wakati wa kujifungua na hizi jitihada zitaendelea ili twende vizuri.
"Zaidi hospitali yetu ya rufaa ina huduma za wagonjwa mahututi, watoto njiti, kusafisha figo huduma ambazo awali hazikuwepo katika mkoa huo," amesema Dk.Samia Suluhu Hassan mbele ya wananchi wa mkoa huo.
Pia amesema katika hospitali hiyo kuna vifaa vya kisasa ambavyo ni CT Scan na X Ray inayomfuata mgonjwa badala ya mgonjwa kupanga foleni kusibiri huduma hiyo.
Ameongeza kuwa kuna huduma za MRI ambazo zinapima magonjwa ya ndani hivyo mkoa huo umejitosheleza kwa huduma za afya.
Mgombea urais Dk.Samia amesema pia kwa kushirikiana na hospitali za kidini ikiwemo KCMC serikali imefanikisha kujenga jengo la mionzi litakalokuwa likitoa tiba ya maradhi ya kansa.
"Kwa sasa mtu wa Kilimanjaro hana haja kwenda Ocean Road Dar es Salaam. Matibabu ni hapahapa Kilimanjaro," amesema.
Dk. Samia amesema katika miaka mitano ijayo Serikali itaendeleza utoaji huduma hizo na kukamilisha maboresho ya hospitali za Moshi, Mwanga na Rombo.
Kwa upande wa upatikanaji dawa katika mkoa huo umefikia asilimia zaidi ya 80 huku dawa muhimu ambazo lazima ziwepo hospitalini zinapatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...