*Atembea kilometa za mraba 947,403 kwa kutembea mikoa yote nchini
*Kihongosi asema CCM imeweka rekodi ya mahudhurio katika
*Kesho ndio funga kazi ikihitimisha kampeni zake katika Jiji la Mwanza
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mwanza
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha kampeni ametembea kilometa za 947,403 kwa kupita maeneo yote nchini huku akiwa amefuatiliwa na watu mara milioni 164.9 jambo ambalo linadhihirisha ukubwa wa chama hicho pamoja kukubalika kwa mgombea wake.
Kimesema katika uchaguzi mkuu mwaka huu CCM pia imeweka rekodi kubwa ya mahudhurio ambayo haijawahi kutoke tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Akizungumza leo Oktoba 27,2015 mbele ya Jukwaa la Wahariri Tanzania pamoja na makundi mengine katika jamii Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Itikadi ,Uenezi na Mafunzo Kenani Kihongosi amesema mpaka sasa watu milioni 25.3 wamehudhuria mikutano yao ya hadhara.
"Watu milioni 57.1 wamefuatilia kampeni zetu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi yetu. Namba za kimtandao zinaonyesha kuwa Dk. Samia katika kipindi cha kampeni amefuatiliwa mara milioni 164.9. Hii inadhuhirisha ukubwa wa CCM lakini kukubalika kwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Akifafanua zaidi amesema leo Oktoba 27 ni siku ya 60 tangu waanze mzunguko wa kampeni zao ni wiki nne na siku nne za makutano ya ana kwa ana baina ya mgombea urais Dk. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote katika mikoa yote aliyopita.
"Ni miezi miwili ya mawasiliano yaliyokuwa na maelewano na masikilizano ya kiwango cha juu kwa sababu mgombea amefanyakazi ya kukutana na wananchi ngazi ya kata, vijiji, vitongoji, wilaya mpaka mikoa.
Amesema “Amekuwa akinadi sera na kuinadi Ilani ya uchaguzi Mkuu ya 2025- 2030 ambapo yamekuwa majuma ya kuwafikia Watanzania popote walipo kuwaomba ridhaa ya kuendelea kuongoza. Muhimu zaidi kuwajengea matumaini mapya kutokana na huduma ya kazi na utu ambayo CCM itawapatia kupitia Serikali ambayo Dk. Samia atakwenda kuiunda.
“CCM katika kipindi hicho kipo salama na afya ya mgombea wetu wa urais ni imara kwani amezunguka kila kona ya nchi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 947,403.Amezunguka na kuzungumza na Watanzania mbalimbali katika maeneo hayo.
“Mgombea urais Dk.Samia yupo timamu na yupo tayari kuendelea kutoa utumishi ndani ya nchi,”amesema Kihongosi huku akisisitiza wameweka rekodi kubwa ya mahudhurio ambayo haijawahi kutoke tangu kuanza kwa vyama vingi mwaka 1992.
Akieleza zaidi amesema pia mamilioni ya Watanzania walijumuika na CCM katika kampeni kwani Chama kinajivunia ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano kwani imekuwa rahisi idadi kubwa ya watu kufikiwa.
"Waliotufuatilia kupitia redio, televisheni, magazeti, mitandao na simu, kompyuta na vifaa vingine vya kidigitali ndani ya vyombo vya usafiri vibanda umiza, Watanzania wengi wametufuatia kwa idadi ambayo haijawahi kutokea.
"Mgombea wetu wameshafanya mikutano zaidi ya 114 ya kampeni yote imekuwa na mafanikio makubwa viwanjani. Msafara wa mgombea wetu Dk. Samia umeweza kusimamishwa maeneo mengi.
"Wananchi wakiwa na shauku ya kumuona mgombea, kumsikiliza na yeye hakusita kuweza kuzungumza na Watanzania pindi alipokuwa akisimamsishwa. Ameonyesha utu wa kuwajali watu anaowahudumia na kuwaomba ridhaa.
“Wingi wa watu waliojitokeza kutaka kumsikiliza Dk. Samia ni tafsiri ya imani kubwa ya watu kwa CCM na upendo mkubwa kwa Dk. Samia kutokana na uongozi wake unaojali utu na matokeo aliyoyaonyesha kwa miaka minne iliyopita.”
Kihongosi amesema katika mikutano hiyo Dk. Samia alinadi Ilani na kutoa ahadi zake, aliwasikiliza wananchi hivyo usikivu huo uliwezesha kuhuhisha ahadi zake kwa muhula ujao.
Amebainisha masuala hayo yamewezekana kwa sababu Dk. Samia anaipenda Tanzania, kujali na kuzingatia kesho ya nchi na kuthamini utulivu wa taifa.
Kuhusu kesho Oktoba 28,2025 amesema kwamba CCM inafanya mkutano wa fungakazi, mkutano wa kihistoria, hivyo amewaalika wananchi waone mambo yanavyofanywa ndani ya CCM.
“Mkutano huo wa fungakazi, utaongozwa na mwanamke shupavu, mahiri na mweledi Dk. Samia Suluhu Hassan. Waliopo mbali wafuatilie kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Imani yetu watanufaika na kujua nini CCM kinauenda kufanya ndani ya miaka mitano inayokuja.
“Ujumbe wangu wenye msisitizo mkubwa Oktoba 29 Mtanzania jitokeze ukapige kura, kitendo chako cha kupiga kura ndicho kinachokuthibitisha kuwa ni raia unayetambua haki na wajibu wako.
“Na unakitumia CCM kikatimize ndoto yako, tunaamini hakuna chama ambacho kimebeba matarajio ya wananchi wa nchi hii tofauti na CCM. CCM ndiyo chama kiongozi, chama chenye sera na ilani inayotekelezeka.”



.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)






.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...