Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Zanzibar

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia.Suluhu Hassan amehutubia maelfu ya wananchi wa Zanzibar alipokuwa akihitimisha kampeni zake katika visiwa hivyo huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura.

Akizungumza leo Oktoba 24,2025 katika Viwanja vya Maisala Mnazi Mmoja Zanzibar akihitimisha kampeni zake upande wa Muungano Dk.Samia amesema zikiwa zimabaki siku chache kufanya uchaguzi wale waliokuwa wakisema Oktoba tuna jambo letu basi jambo liko uwanjani sasa ni kuvaa njumu na kwenda kulitekeleza

"Hatuna budi sote kushiriki kuchagua viongozi tunawaotaka na bila kupepesa maneno tukachague wagombea wa CCM.Twendeni kushiriki uchaguzi bila hofu yoyote kwani vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania viko timamu na viko kamili kuhakikisha usalama wa nchi na raia wake kabla na baada ya Uchaguzi

"Mwito wangu wananchi wote twende tukapige kura,toka tumeanza kampeni viwanja ni tele kwa tele wananchi wamekuja kwa wingi sana.Wingi hautakuwa na maana kama hatujautafsiri ndani ya masunduku,kwenye viwanja tujae lakini na kwenye masunduku yaende yakajae."

Hivyo amesema kila aliyeandikishwa katika daftari la kupiga kura aende kupiga kura huku akiwaomba baba au mama wanapotoka basi hakikisha vijana wao walioandakishwa wanatoka nao.

"Kwa mabalozi wetu kila eneo hakikisha unatoka na mwananchi wako aende kupiga kura,sisi wana CCM hatuna sababu ya kutokwenda kupiga kura ,na ili tufanye hivyo ni vema kutambua kituo chako cha kupiga kura mapema kwa kuhakiki kituo chako,jina lako na wapi umepangiwa kupiga kura ili siku ikifika ni moja kwa moja kwenda kupiga kura.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...