Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kagera
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametaja aina tatu ambazo Serikali imeendelea kusimamia katika kuboresha maisha ya wananchi na kuinua uchumi wa Watanzania.
Akizungumza leo mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera akiendelea na mikutano ya kampeni kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025 Dk.Samia aina ya kwanza ni kukuza na kupeleka kwa wananchi huduma za kijamii.
“Hapa tunazungumzia afya maji, elimu, umeme.Katika hayo tumejitahidi kufanya kwa nchi nzima na kwa Kagera pia tumejitahidi kufanya na tunatambua maendeleo ni safari na ni hatua.
“Kwenye afya tutandelea kujenga vituo vya afya, zahanati na kumalizia hospitali za wilaya katika maeneo ambayo hatujamaliza.Tutaendelea kutoa hudima za dawa za lazima zinapatikana.Vifaa tiba na vitendeakazi vyote vinapatikana, hatuwezi fikia asilimia 100 lakini tulipofikia siyo haba.”
Pia amesema Serikali inaendelea kujenga miundombinu ya elimu VETA na vyuo vya ufundi ili vijana wapate elimu ya ujuzi waweze kujiajiri na kuajiriwa.
“Kwanini tunajenga VETA ni kwasababu tunaangalia mbele nchi yetu inaendelea na viwanda vinakuja, uwekezaji unakuja miradi mikubwa kama bomba la mafuta yatahitaji wafanyakazi.
“Tunamalizia mazungumzo mradi mkubwa wa mchuchuma na liganga kuchimba chuma na makaa ya mawe ,hivyo tunataka mafundi wa fani mbalimbali.Maendeleo ya bandari zetu, reli tunazozijenga zote zinataka mafundi wa aina mbalimbali.
“Tunazidi kutunisha mfuko vijana wanaotoka kidato sita waende vyuoni bila wazazi kuhangaika na hii bila kujali hadhi ya kiuchumi ya kaya.”
Aidha amesema maji ni jambo la lazima kwa binadaamu hivyo Serikali imefanya jitihada zote ambazo zimetumia mabilioni ya fedha zilizotumika kupeleka maji mtu anaweza kushika kichwa.
“Nakwasasa tumeamua hatutumii maji kwa matumizi ya nyumbani pia kwa ajili ya kukuza kilimo chetu na ndiyo maana tunajenga skimu za umwagiliaji maji nchini ili wakulima wazalishe mara mbili kwa mwaka .Tukuze uzalishaji chakula na mazao ya biashara.”
Kuhusu umeme amesema Serikali imejidhatiti kumaliza kadhia ya umeme na kwamba wameshaweka vijiji vyote kama walivyotumwa na Ilani lakini waliamua kuanza kuunganisha umeme katika vitongoji.
“Tupo takribani nusu ya vitongoji vya nchi tunakwenda kumaliza palipobaki lengo letu kila mtanzania atume nishati safi ya umeme.
“Umeme wetu unatoka kwenye vyazo safi maji, upepo, jua na kidogo kwenye gesi kwa hiyo tunajielekeza katika matumizi safi ya umeme kwenye matumizi ya kawada, kupikia na usalama.”
Amefafanua pia kutokana na kuwepo kwa umeme vijana wanaweza kufanyabiasjara zao saa zote na ule utaratibu wa kurudi nyumbani saa 12 kwasababu ya kiza.
“Umeme umefanya siku hizi saa 12 bado ndiyo kumekucha mitaani huko mataa yanawaka hawana shida ya usalama upo.Umeme tumeuweka kwamba ni huduma muhimu kwa wananchi na tutaendelea mkutupa ridhaa.
Akiendelea kufafanua Dk.Samia amesema aina ya pili ambayo Serikali imeendelea kuweka mkazo ni kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Kwanza ruzuku kwenye kilimo kwani kama isingetolewa wakulima wangewajibika kutoa fedha kununua mbolea na hivyo wasingeweza kununua mbolea nyingi, wangenunua kidogo l, wangetumia shambani kidogo ma mazao yangekuwa kidogo.
“Kwa sababu tunawatoza nusu ya bei wanapata mbolea nyingi na wanavuna mazao mengi, wanauza mazao mengi na wanapata pesa nyingi.
“Eneo la pili ni mikopo na kupeleka mitaji kwa wananchi kupitia asilimia 10 ya hamalshauri, Mfuko wa TASAF kuwawezesha wananchi pamoja na mifuko mbalimbali ya mikopo kwa wananchi.
Pia amesema kuwa ujenzi wa stendi na masoko ni kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa sababu katika stendi hizo kuna fursa za kibiashara.
Wakati huo huo katika sekta ya mifugo kuna chanjo kwa wafugaji ambayo Serikali imetoa kwa nusu bei lakini kwa kuku ni bure.
Pia amesema tangu Serikali imeanza kushughulikia zao la kahawa tumekata tozo nyingi na ile fedha iliyosamehewa haikatwi inaingia mfukoni mwa mkulima ni kumwezesha mkulima.
Wakati kundi la tatu ambalo Serikali imeweka mkazo ni sekta za uzalishaji ambazo ni kilimo, viwanda na miundombinu.
“Kwenye usafiri na usafirishaji ni barabara ambapo niwahakikishie zinakwenda kujengwa kwa kiwango cha lami.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...