PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo Oktoba 15,2025 katika kata ya Puma wilaya ya Ikungi ndani ya Jimbo la Ikungi Magharibi mkoani Singida.
Akiwa Katika mkutano huo,Dkt. Nchimbi aliinadi Sera na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2025-2030 kwa Wananchi ikiwemo na kuwaomba kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Aidha,Dkt Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ikungi Magharibi Ndugu Elibariki Immanuel Kingu,mgombea Ubunge jimbo la Ikungi Mashariki Ndugu Thomas Mgonto KITIMA na Madiwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...