Na Pamela Mollel, Arusha
Shirika lisilo la kiserikali Dyslexia Tanzania limeandaa mbio maalumu zijulikanazo kama “Dyslexia Awareness Run”, zenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu watoto wanaojifunza kwa njia tofauti na mfumo wa kawaida unaotumika mashuleni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, mwanzilishi wa shirika hilo Caudence Ayoti alisema kuwa tafiti zinaonesha kati ya watu watano, mmoja hukumbwa na changamoto ya kujifunza, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuelimisha jamii mapema kuhusu hali hiyo.
Ayoti aliongeza kuwa serikali kupitia mtaala mpya wa CB (Competence Based Curriculum) imeanza kuangalia uwezo halisi wa mtoto badala ya mfumo wa zamani uliokuwa ukihimiza kukariri, akisema ni hatua chanya inayofungua nafasi kwa watoto wenye Dyslexia kuonekana na kuthaminiwa.
“Kazi kubwa tunayofanya ni kutoa elimu kwa jamii kuacha kuwaita watoto hawa ‘mazombi’ au kuwadharau. Tunataka jamii iwaoneshe upendo, uelewa na ukaribu,” alisema Ayoti akisisitiza dhamira ya taasisi yake kuendelea na warsha mashuleni na kampeni kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, alibainisha kuwa kupitia mbio hizi, taasisi yake inalenga kuongeza uelewa mpana zaidi, huku akifichua kuwa msukumo wa kuanzisha Dyslexia Tanzania ulitokana na uzoefu binafsi wa kulea mtoto mwenye changamoto hiyo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Dyslexia Tanzania, Snape Mwasyoke, alisema mbio hizo zitafanyika tarehe 19 Oktoba 2025 katika viwanja vya Mgambo jijini Arusha kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, chini ya kauli mbiu “Tupaze Sauti Zetu”, zikilenga kuhamasisha ushiriki mpana wa jamii.
Naye Mwenyekiti wa Riadha Mkoa wa Arusha, Gerald Babu, alisema mbio hizo hazitaishia kwenye uelewa pekee bali pia zitasaidia kuibua vipaji vipya kwa watoto, huku Mkurugenzi wa DEMI Tours, John S. Rashidi, akiongeza kuwa kampuni yake imetenga asilimia 20 ya mapato kusaidia watoto wanaokabiliwa na changamoto za kujifunza kutokana na uelewa mdogo uliopo kwa jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...