
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kulia), akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Oktoba 6,2025 katika ofisi za EWURA jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imerahisisha upatikanaji wa vibali, leseni na utatuzi wa malalamiko kupitia mifumo ya kidijitali, hatua inayowawezesha wananchi kupata huduma popote walipo na kwa wakati bila kulazimika kufika ofisini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja, katika ofisi za EWURA, Dodoma, leo 6.10.2025.
“Tumeendelea kuboresha mifumo yetu ya kidijiti ambayo imeimarisha utoaji wa huduma kwa kasi zaidi na kwa wakati, na kuondoa kabisa malalamiko ya ucheleweshwaji yaliyokuwepo awali” alisema Dkt.Andilile
EWURA inatumia mifumo kadhaa ya kidijiti ikiwamo E- LUC, ambao unasaidia kupokea mrejesho na maoni ya wateja juu ya namna wanavyopokea huduma zinazodhibitiwa kutoka kwa watoa huduma wanaosimamiwa na EWURA. Mfumo huu unapatikana katika aplikesheni ya simu ya kiganjani.
Pia upo mfumo wa LOIS unaorahisisha maombi ya leseni, vibali vya ujenzi wa miundombinu ya bidhaa zinazodhibitiwa pamoja na uwasilishaji wa malalamiko yanayohusu huduma za nishati na maji.
Dkt Andilile amewataka wafanyakazi wa EWURA kuendelea kutoa huduma kwa weledi na kwa wakati ili wateja wake wafurahie zaidi huduma za udhibiti.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kulia), akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja uliofanyika leo Oktoba 6,2025 katika ofisi za EWURA jijini Dodoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa EWURA wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Andilile, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo Oktoba 6,2025 .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...