NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Familia ya Marehemu Yahya Msabila Kafuye wa Mbezi Msakuzi, Wilaya ya Ubungo, imeiomba Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kuwasaidia kutatua mgogoro wa ardhi unaodaiwa kudumu kwa takribani miaka 14.
Akizungumza na vyombo vya habari, mjane wa marehemu, Pilly Kafuye, alisema familia yao imekuwa ikiishi katika eneo hilo tangu mwaka 1977, lakini baada ya mumewe kufariki dunia, mwaka 2014 waliibuka watu wanaodai kuwa wamiliki halali wa ardhi hiyo na kuwaita wao “wavamizi.”
“Tumeishi hapa tangu enzi za mume wangu, tulilinunua eneo hili kihalali. Lakini sasa hivi tunahangaika kwa miaka yote hii bila amani. Tunaomba Rais Samia atuangalie, maana tumechoka kudhulumiwa,” alisema Bi. Kafuye kwa masikitiko.
Baadhi ya majarani wa familia hiyo walioungana kutoa ushuhuda wamesema wameitambua familia ya marehemu kama wakazi halali wa eneo hilo kwa miaka mingi, hivyo wakaiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha haki inapatikana na mgogoro huo unamalizika kwa amani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...