Na Said Mwishehe,Michuzi TV
UMAARUFU wa Mkoa wa Kilimanjaro ni pamoja na uwepo wa Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima wa pili kwa urefu duniani ambao nao Oktoba 1,2025 umetumia muda wake vizuri kufuatilia kwa karibu mkutano wa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk.Samia Suluhu Hassan.
Dk.Samia alifanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa Mashujaa mkoani Kilimanjaro na hakika shughuli mbalimbali za Wakazi wa Mkoa huo wameamua kusimamisha kwa muda ili kuhakikisha wanafuatilia vema mkutano wa kampeni za mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Ukweli ni kwamba kwa akili ya kawaida ni ngumu kuamini kama hata Mlima Kilimanjaro unaweza kufuatilia mkutano wa Dk.Samia, lakini kwa akili ya picha unaona kabisa ni jambo ambalo linawezekana kabisa.

Unajua kwanini?Kwa kawaida Mlima Kilimanjaro umekuwa mgumu kuuona kwa urahisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo hali ya hewa haswa kunapokuwa na mawingu angani.
Kuna sababu nyingi ambazo zimefanya Mlima Kilimanjaro kuonekana vizuri na moja ya sababu ni kwamba katika miaka minne na nusu ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuutangaza utalii wa Tanzania na kupitia Filamu ya The Royal Tour.Ameitendeke haki.
Tunafahamu kupitia filamu ya Royal Tour Rais Dk.Samia alifanikiwa kuutangaza vema Mlima Kilimanjaro na ukweli idadi ya watalii kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni wanaoingia Tanzania ,wanaoingia Kilimanjaro imekuwa kubwa.

Kupitia filamu ya The Royal Tour Rais Samia ameithibitishia dunia tena kwa ushahidi kwamba Mlima Kilimanjaro uko Tanzania na wala sio Kenya. Kwani kulikuwa na ubishani usio rasmi kuwa, mlima huo uko wapi, Tanzania au Kenya?
Lakini Rais Samia hakutumia nguvu kubwa kuuleza ukweli kuhusu mlima Kilimanjaro.Filamu ya The Royal Tour imetosha kabisa kueleza Mlima huo kwamba uko Tanzania.
Hivi sasa Watanzania tumebakia tukishuhudia ujio wa maelfu kwa maelfu ya watalii na kubwa zaidi Serikali imeendelea kupata mapato kutokana na uwepo wa mlima huo katika ardhi ya Tanzania, ardhi ya Kilimanjaro
.

Kwa vyovyoye iwavyo Mlima Kilimanjaro kwa lugha ya picha umeamua kujitokeza kwa uwazi na uzuri kabisa kuufutilia mkutano wa Dk.Samia kwa kuwa nao utambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa sasa anatetea nafasi hiyo urais.
Pamoja na hayo naamini Mlima Kilimanjaro moja ya hamu yake kubwa ni kuona Dk.Samia Suluhu Hasan anatoa muelekeo mpya katika kuendeleza sekta ya utalii nchini na hasa katika kuendelea kuutangaza mlima huo kama ambavyo amefanya katika miaka minne na nusu iliyopita.
Kwa ubunifu ambao Rais Dk.Samia ameufanya katika filamu ya The Royal Tour wala sishangai kuona Mlima Kilimanjaro umekua.

Lakini kwa siku ya leo (Oktoba 1)hali ilikuwa tulivu na kutoa nafasi ya Mlima Kilimanjaro ukionesha upendo wake kwa Dk.Samia ambaye hakika amekuwa rafiki mkubwa wa sekta ya utalii hapa nchini.
Huenda kwa wale ambao wanaotoka nje ya mikoa ya Kaskazini hasa Kilimanjaro na Arusha wanaweza wasielewe nazungumza nini lakini wale wanaotoka mikoa hiyo wanaelewa kuhusu Samia na Utalii.
Ukitaka kujua matokeo chanya ya filamu ya The Royal Tour ngoja nitoe takwimu ndogo tu.Iko hivi, kabla ya Dk. Samia kuingia madarakani Tanzania ilikuwa inaingiza idadi ya watalii milioni moja waliokuwa wanatembelea vivutio mbalimbali.

Hata hivyo ndani ya miaka minne idadi hiyo imeongezeka kufikia watalii milioni tano ambapo siri ya mafanikio hayo ni filamu ya Tanzania Loyal Tour ambayo Dk Samia alikuwa kinara kwenye filamu hiyo.
Pia mafanikio katika sekta hiyo yamechagizwa na mazingira mazuri yaliyowekwa kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo ikiwemo ujenzi wa Hoteli za kisasa.
Aidha, Dk.Samia alipoingia madarakani alihakikisha vikwazo vya kikodi na tozo hususan kwa waongoza watalii na wasindikizaji watalii kupanda Mlima Kilimanjaro vinaondolewa.

Ukweli binafsi sikushangaa kuona mlima Kilomanjaro umetenga muda wake kufuatilia mkutano wa mgombea urais Dk.Samia Suluhu Hassa ambaye amekuwa kinara wa utalii nchini.
Najua kuna watu vichwa ngumu huenda hawajaelewa filamu ya The Royal Tour imeitangaza vipi Tanzania ,nakukumbusha tena filamu hiyo imeitangaza nchi kwasababu hata wakati Dk.Samia anaizindua nchini Marekani, takribani chaneli 350 zilishuhudia uzinduzi wa filamu hiyo.

Lakini baada ya filamu hiyo kuzinduliwa inapatikana katika mtandao wa Amazon na Apple tv ambayo inatumiwa na watu wengi dunia.
Kupitia filamu hiyo watu wengi wamefahamu madini ya Tanzanite yanapatikana nchini Tanzania peke yake na hakuna nchi nyingine inayotoa madini hayo zaidi ya Tanzania.
Hivyo Mlima Kilimanjaro kama nilivyosema awali kwa lugha ya picha kwa niaba ya sekta ya utalii umeona siku ya leo kwa kumpa heshima Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuonekana kwa urahisi.
Halafu sijui watu wanaopanga majukwaa katika mikutano ya kampeni leo kama wamejua vile Mlima Kilimanjaro ulikuwa umekaa upande wa kulia wa jukwaa .
Hakika nami kama binadamu naomba nizungumze na binadamu wenzangu wenye akili kubwa, akili ndogo na ile ya chini huku mtaani tunasema dishi limeyumba hakikika tunajua thamani ambayo umeipa sekta ya utalii.

Lakini thamani ambayo umetoa kwa Mlima Kilimanjaro na naomba leo nijipe kazi ya kuwa
Msemaji wa Mlima Kilimanjaro kwamba ahsante Rais Samia kwa thamani ambayo umeiweka kwa vitendo kwa Mlima Kilimanjaro.
Nikuhakikishie Mlima Kilimanjaro utakupigia kura Oktoba 29 mwaka huu.
Tunajua mlima hauna uwezo wa kupiga kura lakini safari hii utapiga kura kupitia familia yake kubwa ya watu ambao wanategemea mlima huo kuendesha maisha yao kwa namna mbambali.
Yaani ni hivi, wako waongoza watalii katika mlima Kilimanjaro ,wamiliki wa mahoteli ya kulaza watalii, wenye kampuni za utalii,wanaobeba mabegi ya watalii na wadau wote Oktoba 29 kwa niaba ya ndugu na mwanafamilia mwenzao Mlima Kilimanjaro watakwenda KUTIKI kwa Samia.
Imetosha kwa leo
0713833822
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...