Mgombea Ubunge jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama amehitimisha Kampeni zake za kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Vijiji vyote 56 vya Kata 16 katika Jimbo la Peramiho kwa kufanya mkutano mkubwa kampeni katika Kata ya Mpitimbi, Kijiji cha Mpitimbi A kwa kuomba ridhaa ya uongozi wa Chama hicho kwa wananchi kupitia wagombea wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo kesho Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na wananchi katika Kijiji hicho mbele ya mgeni rasmi katika shughuli hiyo Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Bw. Mohammed Halfani, leo Oktoba 28, 2025, Mhagama amewataka wananchi kufanya maamuzi kwa umakini kabla na wakati wa kupiga kura, kwa kukichagua CCM ili kiendelee kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi.
“Serikali ya CCM kupitia ilani hii mpya ya 2025 mpaka 2030 imepanga kujenga shule mpya za sekondari katika kata tano ikiwemo Mpitimbi, pamoja na kuongeza madarasa zaidi ya 500 katika shule mbalimbali ndani ya Jimbo hilo, ambapo Mpitimbi ni miongoni mwa kata zitakazonufaika” amesema Mhagama.
Kuhusu ujenzi wa barabara, Mhagama amesema tayari mkataba wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 110 umeshasainiwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Likuyufusi hadi Mkayukayu, amesisitiza kuwa mafanikio hayo yataendelea ikiwa wananchi watachagua viongozi wa CCM katika ngazi zote.
Akizungumzia sekta ya kilimo amesema zaidi ya wananchi 65,000 wanapata pembejeo za ruzuku na wakazi wa Mpitimbi wananufaika kupitia mpango huo, kutoka laki moja na elfu hamsini kwa mfuko wa mbolea hadi elfu sabini, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja na kuwatafutia masoko ya uhakika.
Aidha, amesema Mgombea Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi ndani ya siku 100 kuanzisha majaribio ya Bima ya Afya kwa Wote ikiwalenga wazee, wajawazito, watoto na watu wenye ulemavu huku Serikali ikiahidi kutoa huduma za matibabu bure kwa watu watakaothibitika kutokuwa na uwezo lengo likiwa ni kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana kwa wote.
Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa Kata ya Mpitimbi Bw. Issa Kindamba, amesema serikali ya CCM imefanikiwa kutekeleza ilani ya 2020–2025 na sasa imekuja na majibu ya changamoto zilizobakia kwa awamu ya 2025–2030. Ametoa wito kwa wananchi kukipa kura ya ndiyo chama cha mapinduzi ili kuendelea kuleta maendeleo katika kata hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Mohamed Halfani, amewahimiza wanachama wa chama hicho kuamka mapema kesho na kwenda kupiga kura mapema na kurudi majumbani kwao kusubiri matokeo, amesisitiza umuhimu wa kutovaa sare au kutumia usafiri wenye alama za chama ili kuepuka kuvunja sheria za uchaguzi.
Kampeni hizo za kufunga zimehitimishwa kwa shamrashamra kubwa, zikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na wananchi wa Mpitimbi, ambapo wananchi walihamasishwa kuwapigia kura wagombea wote wa CCM kwenye ngazi zote za uongozi ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo kwa jamii zote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...