JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watuhumiwa wanne wakiwa na jumla ya vipande 23 vya meno ya Tembo, katika operesheni iliyoshirikisha askari wa Wanyamapori ilioyofanyika wilaya ya Kilombero na Mvomero ikiwa ni mikakati ya Jeshi hilo kuimarisha ulinzi.
Taarifa ya leo Oktoba 19, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama imeeleza kuwa katika tukio lililotokea Oktoba 12, 2025 katika kijiji cha Sagamaganga kata ya Signal wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro, wamekamatwa Ernest Edwini Makali (53) mkulima mkazi wa Mbingu na Loyce Mwaka Luvanda (58) mkulima mkazi wa mkoani Iringa wakiwa na vipande 20 vya meno ya Tembo.
Aidha mnamo Oktoba 13, 2025 katika kitongoji cha Kimbwala kijiji cha Kisaki wilaya ya Morogoro alikamatwa Mongota Lugwasha Jisabu (27) mkazi wa Kimbwala akiwa na Vipande vitatu vya Meno ya Tembo huku Athumani Sadiki Mtai (32) mkulima mkazi wa Kiduwe na Ayoub Zakaria Kasian (18) wakitiwa nguvuni mnamo Oktoba 15, 2025 katika kijiji cha Kidudwe kata ya Mtibwa wilaya ya Mvomero wakiwa na kichwa kimoja cha mnyama Swala.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...