.jpeg)
Akizungumza katika tukio hilo, Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Pwani, Jenifa Shirima, alisema kuwa wameamua kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu ili kutoa elimu na kufanya kazi za kijamii, kama njia ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua tahadhari na kupunguza athari za majanga.
> “Kupitia maadhimisho haya, tunalenga kutoa funzo kwa jamii ili iweze kujifunza namna ya kujikinga na kuchukua hatua za mapema katika kupunguza majanga mbalimbali,” alisema Kamanda Shirima.
Aidha, mbali na kutoa elimu kwa wananchi, maadhimisho hayo yalihusisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira, uchangiaji wa damu, pamoja na kugawa bidhaa kama sabuni, taulo za watoto na vifaa vya usafi kwa wahitaji.
Kwa upande wake, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kibaha, Bwana Amor Mohamed, alitoa shukrani kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwakumbuka na kuwatembelea, akisema hatua hiyo inaonesha moyo wa huruma na kujitolea kwa ajili ya jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...