Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kibamba Angellah Kairuki amewahakikishia wananchi wa mbezi kuwa barabara inayotokea mbezi kupitia mpiji magohe hadi bunju yenye urefu wa zaidi ya kilomita 24 inakwenda kujengwa msimu huu kwa kiwango cha lami hivyo amewataka wananchi hao kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi kwa kukipa ushindi wa kishindo ikifika hapo oktoba 29 mwaka huu

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye mtaa wa mpiji magohe kata ya mbezi jimbo la kibamba jijini Dar es salaam Mgombea ubunge jimbo la kibamba Angellah Kairuki amewahakikishia wananchi hao kuwa barabara hiyo imekuwa ikisuasua lakini endapo watakipatia ushindi chama cha mapinduzi katika msimu huu inakwenda kujengwa kwa kiwango cha lami

Aidha Kariuki amewahakikishia wananchi wa eneo la Msumi kwa babarabara yao yenye urefu wa takribani kilometa 9 ambayo ujenzi wake umeanza itakamilishwa kwa viwango ikiwa na njia za watembea kwa miguu,mitaro ya maji pamoja na taa za barabarani huku pia akiwahakikishia wananchi hao kuwa endapo watamchagua Dokta Samia kuwa Rais,Anjela Kairuki kuwa Mbunge Jimbo la Kibamba na Pius Nyamtori kuwa Diwani Kata ya Mbezi watahakikisha wananchi wananufaika na huduma ya maji safi kupitia tenki la tegeta A

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Kilumbe Nyenda amewahakikishia wananchi kuwa chaguo bora kwa ajili ya maendeleo yao ni kuchagua wagombea wa chama cha mapinduzi ifikapo oktoba 29 kuanzia nafasi ya Rais, Ubunge na Udiwani

Naye Mgombea nafasi ya Udiwani kata ya mbezi pius nyanthuri pamoja na kumuombea kura Dokta Samia  ili aweze kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania na kumwombea Angela Kairuki kuwa mbunge wa jimbo la Kibamba amewahakikishia wananchi kuwa ilani ya chama cha mapinduzi ina sera ambazo zinatekelezeka kwa ajili ya maendeleo













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...