SHIRIKA la kimataifa lisilo la kiserikali linalotoa huduma za afya ya uzazi nchini, Marie Stopes Tanzania, sasa linajulikana kwa jina jipya la MSI Tanzania, huku likiahidi kuendeleza kutoa huduma zake bila mabadiliko yoyote katika utendaji wake.
Akizungumza katika kongamano la afya (Tanzania Health Summit) jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkazi wa MSI Tanzania, Patrick Kinemo, amesema mabadiliko hayo ni ya jina tu na hayataathiri wala kubailisha huduma au utendaji wa shirika, bali yanakusudia kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Tunabadilisha jina kutoka Marie Stopes Tanzania kwenda MSI Tanzania, lakini kazi na huduma zetu zinabaki zilezile. MSI Tanzania imekuwa ikifanya kazi nchini tangu mwaka 1989, na ni miongoni mwa watoa huduma wakubwa zaidi wa afya ya uzazi nchini,” amesema Kinemo.
Kwa mujibu wa Kinemo, takwimu za mwaka 2024 zinaonyesha kuwa asilimia 25 ya watumiaji wote wa huduma za uzazi wa mpango nchini walihudumiwa na MSI Tanzania kwa kushirikiana na serikali, huku asilimia 40 ya wanaume na wanawake waliotumia njia za muda mrefu za uzazi wa mpango walipata huduma hizo kupitia shirika hilo.
MSI Tanzania inatoa huduma zake kupitia njia mbalimbali, ikiwemo huduma za Mkoba zinazofanyika katika vituo vya serikali kwa ushirikiano wa karibu na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI na Wizara ya Afya. Mfumo huu unawawezesha kufikia wananchi walioko maeneo magumu kufikika, kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma.
Shirika pia linaendesha mfumo wa wauguzi waliopachikwa (embedded nurses) katika vituo vya afya vya serikali. Wauguzi hawa hutoa mafunzo kwa watoa huduma wa serikali ili kuimarisha huduma na kuweka uendelevu wa huduma hata baada ya wahisani kutokuwepo.
Kinemo aliongeza kuwa MSI Tanzania pia inafanya kazi katika kuimarisha sekta ya umma, kusaidia vituo vya afya katika ngazi zote kuboresha ubora wa huduma na uimara wa mifumo ya afya nchini
MSI Tanzania pia inamiliki vituo na hospitali za uzazi zinazotoa huduma za afya kwa ujumla kupitia madaktari bobezi .Hospitali hizo hufanya kazi masaa 24, kuhakikisha huduma za dharura zinapatikana kwa wananchi.
Zaidi, shirika linauza bidhaa rasmi za afya ya uzazi kupitia mfumo wa masoko(social marketing), ikiwemo dawa ya Misoprostol, kondomu za kiume za Life Guard na Flame, pamoja na dawa ya dharura ya uzazi wa mpango (BK1).
“Mbinu hii inatuwezesha kuwafikia watu wa makundi mbalimbali nchini, kuhakikisha kila mmoja anapata huduma au bidhaa inayofaa kulingana na mahitaji yake,” amefafanua Kinemo
Shirika pia linaendesha vituo kituo cha huduma kwa wateja (contact centre) inayowezesha kutoa taarifa na rufaa lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya ya uzazi.
Kinemo alisema kuwa MSI Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha wanawake na wanaume wote nchini wanapata huduma bora, salama na nafuu za afya ya uzazi.
“Tunabeba kauli mbiu yetu ya Afya yako, Chaguo lako, Hatma Yako
Karibuni sana MSI Tanzania,” amesema Kinemo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...