Na Pamela Mollel, Arusha
Wapishi wa Tanzania wameungana na wenzao duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mashefu leo, Oktoba 20, 2025, katika hafla iliyofanyika kwenye Chuo cha Taifa cha Utalii (CTA) jijini Arusha. Tukio hilo limehudhuriwa na wapishi maarufu wakiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mashefu Tanzania (Abas Said Omary), mpishi mwenye tuzo za kimataifa Juliana Benjamin Ilanda, pamoja na Shefu Tom, mzoefu katika sekta ya upishi na mwalimu wa mashefu nchini.
Katika maadhimisho hayo, wapishi walitoa mafunzo ya mapishi ya kiafya na lishe bora kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya malezi mkoani Arusha. Lengo lilikuwa kuwajengea watoto uelewa wa lishe bora na kuwahamasisha kupenda taaluma ya upishi. Wapishi hao pia walihimiza matumizi ya mazao ya asili katika mapishi ili kukuza afya na utamaduni wa chakula cha Kitanzania.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Mashefu Tanzania, Abas Said Omary, alisema sekta ya upishi ni nyenzo muhimu ya kukuza afya na uchumi wa taifa. “Kupika si tu kazi ya jikoni, ni taaluma inayogusa maisha ya kila mtu. Kupitia chakula tunajenga afya, uchumi na utu wa jamii yetu,” alisema Omary huku akiwataka wapishi kuendelea kushirikiana na jamii katika kuelimisha kuhusu lishe bora.
Kwa upande wake, mpishi mashuhuri mwenye tuzo za kimataifa, Juliana Benjamin Ilanda, aliwatia moyo watoto na vijana kuichagua taaluma ya upishi kwa kuiona kama sehemu ya ubunifu na fursa ya ajira. “Upishi si kazi ya kawaida, ni sanaa. Ukiwa na kipaji na nidhamu, unaweza kufika mbali duniani,” alisema Juliana, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza vyakula vya asili vya Kitanzania.
Naye Shefu Tom, mzoefu katika sekta ya mapishi na mwalimu wa wapishi, alisema kuna haja ya taasisi za mafunzo kuwekeza zaidi katika vitendo na ubunifu. “Tunapaswa kuwapa vijana nafasi ya kufanya majaribio jikoni, kujifunza kwa vitendo na kutumia malighafi zinazopatikana nchini,” alisema Shefu Tom, akibainisha kuwa hiyo ndiyo njia bora ya kukuza ubunifu wa ndani.
Baada ya mafunzo, watoto walishiriki mashindano madogo ya mapishi ambapo walionesha ubunifu na ujuzi walioupata kutoka kwa mashefu. Mashindano hayo yaliibua vipaji vipya na kuongeza hamasa miongoni mwa watoto. Washindi walipewa zawadi ndogo kama ishara ya kuthamini juhudi zao, jambo lililoongeza furaha na motisha katika tukio hilo.
Maadhimisho hayo yameonyesha namna Siku ya Kimataifa ya Mashefu inavyoweza kuwa chachu ya maendeleo ya jamii kupitia elimu ya lishe na ubunifu. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004 na Worldchefs, siku hii huadhimishwa kila Oktoba 20 kwa lengo la kutambua mchango wa wapishi duniani katika kukuza lishe bora, ubunifu, na ustawi wa kijami

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...