Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Geita

MGOMBEA kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kuimarisha ustawi wa makundi maalum watu wenye mahitaji maalum. 

Akizungumza leo Oktoba 12,2024 mbele ya maelfu ya wananchi wa Jimbo la Geita Mjini mkoani Geitq pamoja na kuzungumza maendeleo yaliyopatikana katika Mkoa huo katika sekta mbalimbali lakini pia Serikali imeendelea kuimarisha ustawi wa makundi yote.

“Ndugu zetu wenye changamoto za ulemavu wa viungo, ulemavu wa ngozi, ulemavu wa kusikia na wenyewe tumeanza kazi kwenye Ilani  hii ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025-2030.

“Pia tunakwenda kuendelea kuwapatia huduma zao kwenye maeneo ya elimu, afya zao, mikopo, ajira, michezo lakini hata uwezo wao wa kuingia katika majengo mbalimbali ya serikali kuweza kutafuta usaidizi majengo yote tunayajenga kiasi ambacho waweze kufika waweze kuhudimiwa.

Katika hatua nyingine Dk.Samia amezungumzia kuhusu Dk. Samia amesema Serikali itaendeleza mbuga ya Burigi Chato na visiwa vya Rubondo pamoja na kudhibiti wanyamapori waharibifu.

"Pia tutapima ardhi na kumilikisha kwenye ilani yetu mpya imesema tunakwenda kupima maeneo yetu ikiwemo ardhi ya wafugaji kutoka hekari milioni 3.4 za sasa hadi hekari milioni sita zitakazomilikishwa kwa wafugaji.

Aliongeza: "Tunakwenda kupima maeneo ya miji, makazi na maeneo ya uwekezaji,”amesema na kuongeza eneo lingine ambalo Ilani ya CCM imeagiza ni kuboresha ustawi wa wananchi katika afya.

Wakati huo huo amesema pia Serikali  itajenga tawi la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) hivyo matibabu ya moyo yatafanyika katika mkoa huo.

Ameongeza kuwa mikoa na nchi jirani na Geita nayo wagonjwa watapatiwa matibabu katika tawi hilo la JKCI.

Pia amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali za halmashauri."Kwa hapa mjini tutaendelea kuboresha hospitali yetu ya wilaya na tutajenga jengo la kuhifadhia maiti.”

Kuhusu sekta ya elimu, Dk.Samia amesema Serikali  yake imejenga shule za sekondari, msingi, vyuo vya ufundi ili vijana waweze kujiajiri au kuajiriwa.

Awali Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Asharose Migiro amesema wananchi wana matumaini makubwa na Dk Samia kwani Mkoa wa Geita umepiga hatua kubwa za maendeleo.

Ameongeza ni Dkkiongozi hodari, jemedari na mwenye maono kwani uongozi wake ni wenye kuleta matokeo.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe mkoani Geita ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko, amesema kwamba  Dk. Samia amewezesha mkoa huo kuimarika zaidi kiuchumi.

Amesema  katika sekta ya nishati Dk. Samia alitoa maagizo kutatua changamoto ya mgao wa umeme hatua ambayo imelifanya taifa kuondokana na changamoto hiyo.

Amesema mkoa huo kwa sasa unapata umeme kutoka Mwanza na Bulyankulu huku mradi wa uzalishaji umeme kutoka bwawa la Rusumo ukikaribia kukamilika.

Pia, amesema  vijiji vyote vya mkoa huo vimefikishiwa nishati hiyo huku nguvu ikielekezwa katika vijiji vitatu vilivyopo maeneo ya kisiwani."Ametuelekeza kila mchimbaji madini kutumia umeme ili kupunguza gharama. Ametuletea sh. bilioni 11 kusambaza umeme kwenye migodi yote.”

Ameongeza atashangaa  kusikia mtu akiuliza kwanini CCM imeshinda. “Tunashinda kwa sababu ya mipango, mgombea wetu yupo kila mahali akiomba kuda, wazazi wapo wanasaka kura, vijana wapo wanatafuta kura."









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...