Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa nyakati tofauti wamewasha umeme katika Shule ya Msingi Julia Wilayani Newala na Shule ya Sekondari Mbawala ya Wilayani Mtwara Mkoani Mtwara kupitia Mradi wa Ujazilizi 2C unaotekelezwa katika Wilaya zote mkoani humo.
Tukio hilo limefanyika kwa nyakati tofauti Oktoba 24, 2025 wakati wa Kampeni maalum inayoratibiwa na REA ya kuelimisha wananchi taratibu za kuunganishiwa umeme na kuwahamasisha kutumia umeme kujiletea maendeleo inayoendelea Mkoani Mtwara.
“Mradi wa Ujalizi 2C unaowashwa leo unatekelezwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara na umelenga kufikisha huduma ya umeme kwenye jumla ya vitongoji 461 na utanufaisha wateja wa awali zaidi ya 20,000,” alisema Msimamizi wa Miradi ya REA Mkoa wa Mtwara, Mha. Daniel Mwandupe wakati anawasha umeme katika Sekondari ya Mbawala.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wa shule hizo waliishukuru REA kwa kuwafikishia mradi na walisema kuwa utakwenda kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na pia utapunguza baadhi ya gharama walizokuwa wakitumia ikiwemo gharama ya kudurufu mitihani na gharama za kukodi taa za sola.
“Umeme utasaidia wanafunzi kupata muda mwingi wa kujisomea kwani hapo kabla tulikuwa tunakodisha taa za sola na zilikuwa zikiwahi kuzima na hivyo wanafunzi kupata muda mchache wa kujisomea na pia tulikuwa tunatumia gharama kubwa,” alisema Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbawala Amina Mtuvenge.
“Tulikuwa tunaishi katika mazingira magumu kwa kukosa umeme, lakini kwa ujio wa mradi utasaidia taasisi yetu kuandaa mambo mengi ikiwemo kuwa na vipindi vya ziada mida ya jioni, kutumia vifaa vya Sanaa ambavyo vinahitaji umeme kujifunzia sambamba na kuanza kutumia vifaa vya Tehama,” alisema Salum Mawazo Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Julia.
Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hizo walisema kufika kwa umeme shuleni hapo kutawaongezea muda wa kujisomea kwa kuweza kurudi shuleni mida ya jioni lakini pia kutasaidia wao kupata elimu ya matumizi ya Tehama.
“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea umeme kupitia mradi wa REA, umeme utatusaidia kujisomea wakati wa usiku tofauti na hapo zamani, wanafunzi waishio hapa shuleni utawasaidia kujisomea wakati wa usiku na hii itasaidia kuongeza ufaulu katika mitihani,” alisema Rashid Kiangazi mwanafunzi wa Kidato cha Tatu.
“Tulikuwa tunakosa fursa nyingi kwa kukosa umeme, ulinzi na usalama mdogo mida ya jioni kukaa maeneo ya shule na muda mchache wa kujisomea lakini kufika kwa umeme kutatusaidia kufaulu tutasoma mida ya jioni na tutaanza kusoma masomo ya Tehama,” alisema Hairath Seleman Mwanafunzi wa Darasa la Tano.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...