Chuo cha Taifa cha Utalii NCT Kampasi ya Arusha kimefurika ari, tabasamu na matumaini mapya baada ya wanafunzi na wakufunzi kuannza rasmi safari yao kupitia programu ya learning for life, ushirikiano kati ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Na NCT unaolenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ujuzi wa vitendo katika sekta ya ukarimu na utalii.
Zaidi ya vijana 160 wamejiunga na kundi hili jipya la mafunzo, wakiwa na hamasa kubwa ya kujifunza na kubadili ndoto zao kuwa uhalisia.
Tangu siku ya kwanza, vyumba vya madarasa na maeneo ya mafunzo yamejaa nishati chanya, ushirikiano na hamu ya kujifunza.
Wanafunzi wanajifunza huduma kwa wateja, uandaaji wa vinywaji (mixiology), na uongozi, yote yakiwa yamelenga kuwaandaa kwa ajira katika hoteli, migahawa na baa kwenye ukanda wa kaskazini wa utalii.
Kwa wanafunzi wengi, programu hii ni zaidi ya mafunzo, ni nafasi ya kujiamini, kukuza taaluma na kufungua milango ya mafanikio katika maisha Wakufunzi nao hawakubaki nyuma katika furaha hii.
Kupitia mfumo wa Training of Trainers (ToT) unaofadhiliwa na SBL, walimu wa NCT wamewezeshwa kutoa mafunzo ya kiwango cha juu yanayochanganya nadhria na vitendo, kuhakikisha kila mwanafunzi anaondoka akiwa tayri kwa soko la ajira.
Kadri mafunzo yanavyoendelea, jambo moja limekuwa wazi, ari bidii na mshikamano vinavyoonekana NCT Arusha ni ishara ya mustabali mzuri wa sekta ya ukarimu nchini Tanzania.
Kupitia ushirikiano huu, SBL na NCT hawatoi tu mafunzo, wanaunda kizazi kipya cha vijana wenye uwezo wa kuhudumia, kuongoza na kuhamasisha wengine.
Zaidi ya wanafunzi 160 wa awamu ya pili wa Programu ya Learning for Life wakisikiliza kwa makini mafunzo yao kwa siku ya kwanza ndani ya Chuo cha Utalii cha Taifa -Kampasi ya Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...