Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa imejizatiti kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu ya ufundi stadi yenye umahiri, ujuzi na ubunifu unaokidhi mahitaji ya soko la ajira la sasa na la baadaye.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo katika ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), uliowakutanisha wamiliki wa viwanda, waajiri na wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi, Prof. Nombo alisema mkutano huo ni jukwaa muhimu la kujadili namna ya kuimarisha nguvu kazi ya Taifa.

"Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 60 ya vijana wako barani Afrika. Hivyo, ni wajibu wetu kuwaandaa vizuri ili waweze kutumika katika soko la ajira la ndani na kimataifa," alisema Prof. Nombo.

Alibainisha kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (toleo la 2023) imeweka mkazo wa kujenga mfumo wa elimu unaolenga ujuzi na tija, huku serikali ikiendelea kuimarisha miundombinu ya mafunzo ya ufundi kwa kuongeza idadi ya vyuo na programu za mafunzo kwa vitendo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Clotilda Ndezi amesema kuwa msukumo mkubwa kuhakikisha mafunzo ya ufundi nchini yanakuwa ya vitendo zaidi, ili kuwazalisha wahitimu mahiri wanaoendana na mazingira halisi ya kazi.”

Ndezi alisisitiza umuhimu wa mitihani ya vitendo, ushirikiano kati ya taasisi za mafunzo na viwanda, pamoja na kutoa fursa kwa wakufunzi kujifunza teknolojia mpya katika maeneo ya kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, alisema taasisi hiyo inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita, ikiwa ni pamoja na ongezeko la vyuo kutoka 37 hadi 80 vinavyotoa huduma, huku vingine 65 vikiwa katika hatua ya kukabidhiwa.

"Tunatambua kwamba serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaipa kipaumbele elimu ya ufundi stadi. Ushirikiano wa wadau ni muhimu ili tuweze kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira," alisema Kasore.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, alihitimisha kwa kueleza kuwa sekta ya viwanda haiwezi kukua bila kuwa na nguvu kazi yenye ujuzi, hivyo serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya elimu ya ufundi stadi kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa Wizara hiyo ni itafanya kuwa wadau wakubwa katika kushirikiana na VETA katika kuhakikisha viwanda vinakuwa nguvu kazi yenye tija.


Matukio katika picha ya ufunguzi wa mkutano wa VETA na Wamiliki wa viwanda na waajiri uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...