Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akizungumza wakati akifungua Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika leo Oktoba 15,2025 katika ukumbi wa The New Kiboko, jijini Tanga.

Na.Mwandishi Wetu-Tanga

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kulinda haki za walaji na kudhibiti bidhaa bandia kupitia Tume ya Ushindani (FCC) ambayo ina mchango mkubwa katika kukuza viwanda nchini na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora, salama na zenye bei stahiki.

Akizungumza jijini Tanga wakati akifungua Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika katika ukumbi wa The New Kiboko, Tanga Ltd Oktoba 15,2025, Dkt. Abdallah alisema semina hiyo imelenga kuongeza uelewa wa watendaji katika kuhakikisha masoko nchini yanabaki na ushindani wa haki unaowezesha maendeleo endelevu ya sekta ya viwanda na biashara.

Aidha, Dkt. Abdallah alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa miongozo yake ya kukuza sekta ya viwanda na biashara huku akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ushindani yanayochochea ubunifu na ukuaji wa sekta ya viwanda.

Pia ameipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa kupata Cheti cha Ithibati cha Ubora (ISO Certificate 9001:2015), hatua hii ni ishara ya utoaji huduma zenye viwango vya kimataifa na hatua hiyo itaimarisha imani ya wadau na wawekezaji nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, amesema FCC inaendelea kufanya doria na ukaguzi katika masoko kwa lengo la kuhakikisha bidhaa zinazouzwa zinakidhi vigezo na hadhi ya soko na kupunguza bidhaa bandia na kulinda afya na maslahi ya walaji.

Naye, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Sempeho Manongi, amesema kuwa semina hii itasaidia Menejimenti ya Wizara na FCC kuelewa kwa kina sheria za ushindani, kumlinda mlaji na mbinu za kudhibiti bidhaa bandia katika mazingira ya sasa ya biashara ya kidijitali.

Vilevile, Mkurugenzi wa Tafiti Muungano ya Makampuni na Utoaji wa Elimu Bi. Zaytun Kikula amesema, ni muhimu kwa Menejimenti ya Wizara kujua sheria zinazohusiana na majukumu makubwa ya FCC katika kuhakikisha Soko linaimarika na walaji wanapata bidhaa sahihi ili kusimamia vyema taasisi zake na kutoa ushauri wa kisera unaozingatia maslahi ya walaji na maendeleo ya sekta ya viwanda nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akizungumza wakati akifungua Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika leo Oktoba 15,2025 katika ukumbi wa The New Kiboko, jijini Tanga.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa,akizungumza wakati wa Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika leo Oktoba 15,2025 katika ukumbi wa The New Kiboko, jijini Tanga.

Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (hayupo pichani) wakati akifungua Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika leo Oktoba 15,2025 katika ukumbi wa The New Kiboko, jijini Tanga.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina ya Uhamasishaji wa Masuala ya Ushindani, Kumlinda Mlaji na Udhibiti wa Bidhaa Bandia iliyofanyika leo Oktoba 15,2025 katika ukumbi wa The New Kiboko, jijini Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...