Dar es Salaam,28-10-2025

Tanzania Bloggers Network (TBN) inatoa pongezi za dhati kwa Watanzania wote, wagombea, vyama vya siasa, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na wadau wote kwa kukamilisha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika mazingira ya amani na utulivu yaliyotawala kote nchini.

TBN inatambua na kupongeza juhudi kubwa zilizofanywa na washiriki wote katika kipindi chote cha kampeni, ambapo hakukuwa na matukio makubwa (vituko) ambayo yangehatarisha amani na umoja wa taifa letu.

Tunasifu tabia ya washiriki kufuata kikamilifu sheria, kanuni, na taratibu zote za uchaguzi, zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi, ikiwemo Kanuni za Maadili (Code of Conduct). Kuzingatia sheria hizi ndio nguzo kuu ya uchaguzi huru, wa haki na wa amani.

"Amani yetu ni urithi na hazina kubwa. Mwenendo wa kampeni za mwaka huu umethibitisha kwamba Watanzania wanaiweka amani na maslahi ya taifa mbele ya tofauti za kisiasa."

Kwa niaba ya wanachama wake wote, TBN inatumia fursa hii kutoa wito kwa kila Mtanzania mwenye haki ya kupiga kura kwamba Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kesho Jumatano, Oktoba 29, 2025, ambayo imetangazwa rasmi kuwa ni Siku ya Mapumziko, kwenda kupiga kura.

Tunawahimiza wananchi wote waliojiandikisha kutumia siku hii ya mapumziko kama fursa ya kipekee ya kufanya mabadiliko wanayoyahitaji katika uongozi kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Kura yako ni sauti yako ya kuweka msingi wa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.

Aidha Tunasisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha amani na umoja na kuzingatia kikamilifu sheria zote za uchaguzi wakati wa kupiga kura na kusubiri matokeo.

Tanzania Bloggers Network (TBN) inawatakia Watanzania wote uchaguzi mwema na wa mafanikio, tukitarajia matokeo yatakayojenga matumaini makubwa kwa taifa hili katika safari yake ya kuelekea maendeleo endelevu.



Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

Mungu bariki Amani yetu.




Beda Msimbe

Mwenyekiti Tanzania Bloggers Network (TBN)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...