Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 6 hadi 11, 2025, Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Ruvuma limeendelea kuwafikia wananchi kwa huduma za moja kwa moja, elimu ya matumizi bora ya nishati, pamoja na kufunga mita janja (Smart Meters) kwa baadhi ya wateja wake wa Manispaa ya Songea bila gharama yoyote.
Zoezi hilo ni sehemu ya mkakati wa TANESCO wa kuboresha huduma na kutumia teknolojia ya kisasa ili kurahisisha maisha ya wateja wake, Mita hizo janja zimeundwa kwa mfumo unaomwezesha mteja kununua umeme na kupokea umeme moja kwa moja kwenye mita bila kuhitaji kuingiza tokeni.
Akizungumza Mhandisi Boniface Malibe kutoka TANESCO Mkoani Ruvuma ameeleza kuwa shirika hilo linaendelea na juhudi za kubadilisha mita za zamani na kufunga mita za kisasa ambazo zinarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakati, kupunguza usumbufu kwa wateja na kuongeza ufanisi wa mfumo mzima wa huduma ya umeme.
“Mita hizi ni za kisasa hazihitaji kuingiza tokeni, Mteja akinunua umeme kupitia simu au wakala, umeme unaingia moja kwa moja, Ni rahisi, salama na ya kisasa zaidi."
Katika kuendeleza uhusiano na wateja, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Alan Njiro, amewahamasisha wananchi kuachana na matumizi ya vifaa vya umeme vya mtumba ambavyo alisema vimesababisha ongezeko la matumizi ya umeme majumbani kutokana na ufanisi mdogo wa teknolojia ya zamani.
Alieleza kuwa tafiti zinaonyesha kuwa vifaa vya umeme vipya na vya kisasa vinatumia umeme kwa kiwango kidogo na ni rahisi kumudu, hivyo matumizi ya vifaa vya mtumba si tu vinawagharimu wananchi bali pia vinaathiri huduma kwa ujumla.
“Zamani watu waliogopa kutumia umeme kupikia, lakini sasa umeme ni nishati nafuu zaidi, ni salama kwa afya, rafiki kwa mazingira na ni rahisi kutumia."
Katika soko la Bombambili, ambapo TANESCO iliweka banda la maonesho ya namna ya kupika kwa kutumia umeme, wananchi walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo namna ya kupika kwa kutumia majiko ya umeme, Mariam Shaibu Mfaume mfanyabiashara katika soko hilo, alikuwa mmoja wa walionufaika na elimu hiyo.
Amesema alipata nafasi ya kupika kwa kushirikiana na wananchi wengine waliotembelea banda hilo ikiwemo wali, ugali, nyama na mboga kwa kutumia majiko ya umeme, na alishangazwa na kasi ya majiko hayo, ameahidi kuanza kuweka akiba kidogo kidogo ili aweze kununua jiko la umeme kwa matumizi ya nyumbani na biashara yake.
TANESCO pia imetumia nafasi hiyo kutoa elimu kuhusu ulinzi wa miundombinu ya shirika hilo, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya kilimo, Afisa wa Kitengo cha Usafirishaji Mariam Abdul, ameeleza kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari wakati wa uchomaji wa mashamba kwa kuhakikisha hawachomi karibu na nguzo za umeme.
Alisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuchorea visahani kwenye maeneo yaliyo na nguzo ili kuzuia moto kufikia miundombinu, jambo ambalo limekuwa likisababisha kukatika kwa huduma ya umeme.
TANESCO Mkoa wa Ruvuma kupitia wiki hii ya huduma kwa wateja imeonyesha kwa vitendo dhamira ya kuwa karibu na wananchi, kusikiliza changamoto zao na kuwatatulia kwa haraka, huku ikisisitiza matumizi bora ya nishati safi ya kupikia ya umeme.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...