Na Farida Mangube, Morogoro
Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO SACCOS) kimefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 27.2 kwa wanachama ikiwa ni sehemu ya mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 57 wa TANESCO SACCOS, uliofanyika Mjini Morogoro, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO SACCOS, Omary Shabani, alisema hadi kufikia Agosti 31, 2025 mikopo hiyo imetolewa kwa wanachama 4,031 waliotimiza vigezo vilivyowekwa na chama.
“TANESCO SACCOS imeendelea kuwa nguzo muhimu ya kiuchumi kwa wanachama wetu. Tumetoa mikopo ya zaidi ya bilioni 27.3 kwa mwaka huu 2025 hatua inayothibitisha dhamira yetu ya kuwawezesha wanachama kifedha,” alisema Shabani.
Kwa upande wake Antony Mbushi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, alisema TANESCO inajivunia uwepo wa SACCOS hiyo, ambayo imekuwa chachu ya kuinua hali ya maisha ya wafanyakazi wa shirika hilo
“TANESCO SACCOS imekuwa mfano bora wa ushirika unaofuata taratibu, sera na misingi ya kisheria katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wanachama. Shirika litaendelea kuunga mkono juhudi hizi,” alisema Mhandisi Mbushi.
Aidha, Shabani aliongeza kuwa pamoja na mafanikio ya utoaji mikopo, SACCOS imewekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi na uwekezaji wa hisa zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10, hatua inayolenga kuongeza mapato na kudumu kwa ustawi wa chama hicho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...