Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuendelea kujenga miundombinu ya kisasa katika bandari zake na kuendelea kutoa huduma za kiwango cha kimataifa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya mtoa huduma jijini Dar es Salaam tarehe 06 Oktoba, 2025, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mkeli Mbossa amesema utendaji kazi wa Mamlaka umeboreshwa ili kuwahudumia wateja kwa ufanisi zaidi.
“Kama sehemu ya mkakati wetu wa kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, tumejipanga kujenga miundombinu ya kisasa katika Bandari zetu na kuendelea kutoa huduma za kiwango cha kimataifa ili kuongeza ufanisi wa uhudumiaji wa shehena,” amesema
Bw. Mbossa ameongeza kwamba kwa kushirikiana na waendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, kampuni ya DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL), Bandari hiyo sasa inatoa huduma bora zaidi na za kisasa.
Amesisitiza kwamba ushirikiano huo pamoja na maboresho ya miundombinu, ndivyo vilivyopelekea kuongezeka kwa shehena ya mzigo kutoka tani milioni 15 kwa mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani milioni 27.8 kwa mwaka 2024/2025
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...