Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo, uliandaa mkutano wa kuwashirikisha taarifa mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya mazingira ya ufadhili na uwezekaji katika miradi ya maendeleo na hatua zinazohitajika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.


Mkutano huu uliwakutanisha viongozi wa serikali, mashirika ya kimataifa, balozi, sekta binafsi na asasi za kiraia, kwa lengo la kujadili njia za kutafsiri malengo ya kitaifa kuwa matokeo halisi kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Balozi Kaganda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya ufadhili wa maendeleo. 


Alieleza kuwa dunia kwa sasa inatumia zaidi ya dola trilioni 2.7 kila mwaka kwa masuala ya usalama, ambapo kiasi kidogo cha pesa hiyo kinatosha kumaliza njaa na kutoa

huduma za afya kwa wote duniani.


“Huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa pamoja na kuendana na Dira ya maendeleo ya Tanzania ya 2050. Kupitia mifumo mipya ya ufadhili wa maendeleo kama vile matumizi ya raslimali za ndani, ushirikishwaji wa sekta binafsi, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, na matumizi ya hati fungani za kijani na za manispaa, tunaweza kuleta maendeleo jumuishi na yanayostahimili mabadiliko ya tabianchi” alisema Mhe. Kaganda.


Dkt. Fred Msemwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, alieleza kuwa Dira ya 2050 inalenga kuiweka sekta binafsi kama injini ya uchumi, huku serikali ikichukua nafasi ya kuwezesha na kupunguza hatari kwa wawekezaji.


Kwa upande wake Bi. Susan Nyamondo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa maarifa yaliyopatikana katika mkutano huo yatasaidia kuoanisha vipaumbele vya serikali na mikakati ya washirika wa maendeleo. Alitoa mfano wa hati fungani ya kijani ya Tanga UWASA kama mfano wa jinsi ubunifu katika miradi ya maendeleo unavyoweza kusaidia kufanikisha malengo ya nchi.


Mkutano ulihusisha pia mjadala ambapo kati ya wana jopo alikuwepo Bwana John Viner kutoka Ubalozi wa Sweden alieleza kuwa mwelekeo mpya wa misaada ya maendeleo waSweden unalenga kusimamia zaidi matumizi bora ya rasilimali na matumizi ya dhamana ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi. 


Bwana Samwel Kilua, Mkurugenzi wa Gatsby Africa-Shirika linalojihusisha na kutengeza  jira na ukuaji wa Uchumi, alisisitiza kuwa washirika wa maendeleo wanapaswa kuzingatia mazingira halisi ya Tanzania na kuongeza thamani

kwenye miradi iliyopo badala ya kufanya kazi kwa kujitenga.


Mkutano huo pia uliangazia mafanikio ya miradi ya UNCDF nchini Tanzania, ikiwemo miradi ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi, kusaidia biashara ndogo na za kati kifedha, kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, na uwekezaji katika mifumo ya chakula ya kilimo. Pia ulionyesha mifumo kiubunifu ya ufadhili kama hati fungani za kijani, uwekezaji

unaozingatia viwango, na LoCAL.


Washiriki walihimizwa kuendeleza ubunifu, kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi, na kupanua miradi iliyofanikiwa ili kuleta maendeleo jumuishi na endelevu. Kadri Tanzania inavyoelekea kuwa nchi yenye kipato cha juu, ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo utakuwa muhimu sana katika kufanikisha Dira ya 2050.

KUHUSU UNCDF UNCDF ni taasisi ya Umoja wa Mataifa inayotoa ufadhili wa maendeleo kwa nchi maskini

zaidi duniani. Lengo lake ni kusaidia nchi hizi kufikia ukuaji endelevu na jumuishi kamailivyoainishwa katika Ajenda ya Maendeleo ya 2030 na Mpango wa Doha wa mwaka 2022–

2031.


UNCDF hufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine ya UN, sekta binafsi na ya umma, kwa kutumia mchanganyiko wa msaada wa kiufundi, ushauri wa sera, mitaji ya uwekezaji, na uhamasishaji wa rasilimali. Kipaumbele chake ni katika maeneo kama uchumi wa kijani, kidigitali, miji, usawa wa kijinsia, na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.













 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...