-Wananchi watahadharishwa kuepuka vishoka
WENYEVITI wa Serikali za vijiji na vitongoji Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara wamesema hawatakuwa na huruma kwa watakaobainika kuhusika na hujuma ya miundombinu ya umeme na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Wamesema hayo Oktoba 21,2025 wilayani humo kwa nyakati tofauti katika vitongoji vya Tripoli, Matogoro, Mpakani B, Mji Mwema na Mnianda wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme inayoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
“Tumepokea mradi wa umeme na ni kama lulu hatukutarajia, tutasimama imara kuhakikisha tunailinda miundombinu hii ya umeme ili isihujumiwe, isiharibiwe na wahalifu wachache wasiopenda maendeleo na amani ya vitongoji vyetu,”amesisitiza Mohamed Malota Mwenyekiti wa Kitongoji cha Matogoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa vitongoji wilayani Tandahimba.
Malota ameishukuru Serikali kwa kutimiza majukumu yake kwa wananchi na aliahidi kwa kushirikiana na wenyeviti wengine watahakikisha umeme unabadilisha maisha ya wananchi kwa kuwahamasisha kuutumia kujiletea maendeleo.
“Rai yangu kwa wananchi, mradi umefika muda mwafaka ni kipindi cha mavuno ya korosho sasa hivi, tuchangamkie fursa hii ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya 27,000 pekee ili tubadilishe maisha yetu,”ametoa wito Matola.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mji Mwema, Abdallah Hassan amewatahadharisha wananchi na kuwataka kuwa makini ili kuepuka kutapeliwa na vishoka wenye kuomba fedha kwa mwananchi ili wamfanyie mpango wa kuunganishiwa umeme na badala yake wafuate taratibu zilizoelekezwa na wataalam kutoka REA.
“Pasitokee mtu yoyote akawadanganya mumpe fedha, huo ni ukorofi na ni utapeli, hata Mwenyekiti mimi sihusiki na suala la mtu kuunganishiwa umeme sina mamlaka hayo kazi yangu mimi ni kushawishi Serikali kuleta mradi ukishafika kazi yangu imekwisha,” alitahadharisha Hassan
Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa vitongoji hivyo walipongeza na kuishukuru Serikali kwa kuwaletea mradi huo ambao walisema unakwenda kubadilisha hali ya maisha yao.
"Sisi wanawake wa kitongoji cha mtogoro tunashukuru kwa huu mradi, tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuondolea giza, ametukomboa sisi akina mama wa hali ya chini, ametuondolea kero nyingi ikiwemo matumizi ya nishati isiyo safi,” alisema Sophia Ali mkazi wa Kitongoji cha Matogoro
Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika kampeni hiyo walisema kuwa kufika kwa umeme katika kitongoji chao kutakwamua hali zao za maisha hasa ikizingatiwa kuwa wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kujiongezea vipato.
“Tulikuwa tunapata shida hata kuchaji tu simu ilikuwa hadi twende mbali lakini kufika kwa umeme mambo yanakwenda kuwa mazuri mimi ni mbanguaji korosho maarufu hapa, tutatumia umeme kubangulia korosho tutaungana akina mama hapa na kuwa na mashine inayotumia umeme kubangua korosho,” alisema Shahara Mwandazi.
“Ninamshukuru Mama Samia kwa kuwatuma REA kutoka huko Dodoma hadi hapa Tandahimba mwisho wa Tanzania, tumeipokea REA kwa furaha, Mama Samia Mungu atakulipa kwa kuwatuma REA kufika hapa, hakika unatujali sana wananchi wako,” alisema Salima Mtawampa Mkazi wa Kitongoji cha Tripoli.
REA inafanya kampeni ya kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme sambamba na kuhamasisha kuutumia kujiletea maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...