Na Diana Byera_Bukoba

Mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kampeni mkoani Kagera tarehe 15 na 16 Oktoba 2025 kwa ajili ya kuomba ridhaa ya wananchi wa mkoa huo kumpigia kura katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bukoba, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Nazri Karamagi, amesema Dk. Samia atafanya mikutano mitatu ya kampeni katika wilaya za Muleba, Missenyi na Karagwe siku ya tarehe 15 Oktoba.

Kwa mujibu wa Karamagi, tarehe 16 Oktoba, mgombea huyo atahitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ambapo atazungumza na wananchi na kuwaombea kura wagombea wa ubunge na udiwani wa CCM mkoani humo.

“Tunatoa wito kwa wananchi wote wa Kagera kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Dk. Samia, ambaye licha ya kuwa ametekeleza mambo mengi mazuri akiwa Rais, anakuja sasa kama mgombea kuomba ridhaa yenu tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano,” 

Ameongeza kuwa mikutano hiyo itatoa fursa kwa wananchi kufahamu sera na ilani ya CCM kwa kipindi cha 2025 hadi 2030, ili kufanya uamuzi sahihi wa kumpigia kura mgombea huyo pamoja na wagombea wengine wa chama hicho.

Ziara hiyo imezua hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera hususan mjini Bukoba, ambapo maandalizi ya kumpokea mgombea huyo yanaendelea kwa kasi, yakiratibiwa na mabalozi wa mashina, wagombea, na viongozi wa chama.

Katika mikutano ya kampeni na harakati za kuomba kura nyumba kwa nyumba, viongozi wa CCM wamekuwa wakihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatano kwenye Uwanja wa Kaitaba kumsikiliza Dk. Samia na kufahamu mwelekeo wa chama hicho kwa miaka ijayo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...