Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

WAZIRI wa Fedha, Balozi Hamis Omar, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 18 ya Chuo cha Kodi (ITA) yatakayofanyika chuoni hapo katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kesho Novemba 21, 2025 mbapo jumla ya wahitimu 561 watatunukiwa vyeti, stashahada, shahada na stashahada ya uzamili.

Akizungumza leo, Novemba 20, 2025 kuhusu maandalizi ya mahafali hayo, Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Isaya Jairo, amesema kati ya wahitimu hao, 317 ni wanaume na 244 ni wanawake.

Aidha, amesema chuo hicho kimeshuhudia ongezeko la wahitimu 144 kwa mwaka wa masomo 2024/2025, sawa na asilimia 30 kutoka wahitimu 417 mwaka 2023/2024.

“Pamoja na kutunuku vyeti, mgeni rasmi atatoa zawadi kwa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea na masomo waliofanya vizuri zaidi katika masomo, pamoja na wahadhiri wa chuo walitoa machapisho mbalimbali. Katika idadi hiyo, wahitimu 256 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha wa Afrika Mashariki (EACFFPC),” amesema Profesa Jairo.

Ameongeza kuwa wahitimu 47 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM), 26 Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (DCTM), 214 Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na 18 Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).

Profesa Jairo amesema cchuo hicho tayari kimefanikiwa kutoa mafunzo kidijitali kwa jumla ya watu 5000 na kinaendelea kujiimarisha zaidi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

“Chuo pia kinajivunia utekelezaji mzuri wa mpango mkakati wa tano wa chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya teknolojia pamoja na kutekeleza kwa ufanisi mpango wa mafunzo ya lazima kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watumishi wapya wa TRA walioajiriwa hivi karibuni,” alisema.

Amebainisha kuwa tayari watumishi 2000 wamepatiwa mafunzo hayo na ushirikiano wa chuo hicho na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Chuo Muster kutoka Ujerumani katika Shahada ya Uzamili unaendelea.

Mahafali hayo yatahudhuriwa na wageni kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo Comoro, Malawi na Zambia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...