-𝐀𝐬𝐢𝐬𝐢𝐭𝐢𝐳𝐚 𝐔𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐧𝐚 𝐔𝐬𝐢𝐦𝐚𝐦𝐢𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐌𝐚𝐳𝐢𝐧𝐠𝐢𝐫𝐚 𝐡𝐚𝐬𝐚 𝐮𝐝𝐡𝐢𝐛𝐢𝐭𝐢 𝐰𝐚 𝐤𝐞𝐥𝐞𝐥𝐞 𝐜𝐡𝐚𝐟𝐮𝐳𝐢 𝐦𝐚𝐞𝐧𝐞𝐨 𝐲𝐚 𝐦𝐚𝐤𝐚𝐳𝐢
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange, amefanya ziara yake ya kwanza katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kuzungumza na watumishi wa Baraza hilo, akitoa maelekezo mahsusi juu ya kuimarisha usimamizi wa mazingira nchini.
Katika hotuba yake, Dkt. Dugange amesisitiza umuhimu wa kulinda afya ya jamii kupitia udhibiti wa kelele chafuzi, akibainisha kuwa kelele zimekuwa chanzo cha changamoto za kiafya, hususani magonjwa yasiyoambukiza katika maeneo ya makazi.
Amesema kelele chafuzi ni miongoni mwa mambo yanayoashiria uharibifu wa mazingira na yanapaswa kudhibitiwa kwa nguvu na umakini wa hali ya juu.
Akiweka msisitizo zaidi, Dkt. Dugange ameagiza NEMC kuandaa mpango mkakati wa mashirikiano kati yake na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hasa kwenye majiji ili kuhakikisha udhibiti wa kelele chafuzi unatekelezwa katika ngazi zote kutoka Mtaa hadi Taifa.
Amesisitiza kuwa kila mtumishi wa NEMC ana jukumu la kuhakikisha jamii inajengewa uelewa na Sheria za Mazingira zinatekelezwa ipasavyo.
Katika mazungumzo hayo, Dkt. Dugange pia ameuzungumzia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2050 unaohusisha nguzo tatu kuu, ikiwemo Uhifadhi wa Mazingira na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi
Amefafanua uhusiano uliopo kati ya mazingira salama, afya bora, na kupungua kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Akigusia ajenda ya nishati safi, Dkt. Dugange alikumbusha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inataka ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ambayo ina manufaa kwa jamii ikiwemo kupunguza uchafuzi wa hewa, kulinda mazingira na kupunguza gharama za maisha.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Mhandisi Mwanasha Tumbo, ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo yote yaliyotolewa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Immaculate Sware Semesi amepokea maelekezo na kuahidi kuyatekeleza kwa mujibu wa Sheria na kuhakikisha usimamizi thabiti wa mazingira nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...