Na Kassim Nyaki, Karatu.
Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameelekeza taasisi za uhifadhi kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori ili kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.
Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo leo tarehe 28 Novemba, 2025 wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakati wa ziara ya kujitambulisha kwenye taasisi na kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.
Katika kikao hicho Mhe. Waziri Kijaji ameelekeza kuwa kila taasisi ni lazima iwekeze kwenye teknolojia za kısasa ili kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ambazo ni kichocheo cha wageni mbalimbali kutembelea nchi yetu.
Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Hamad Hassan Chande amewataka watumishi katika sekta ya uhifadhi na utalii kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu katika kuwahudumia wageni.
Akiwatambulisha viongozi hao kwa menejimenti ya Ngorongoro Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuharakisha mipango ya serikali inatekelezwa.



.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...