Na Mwandishi Wetu
JUBILEE Insurance (Jubilee Life na Jubilee Health) leo Novemba 17,2025 wamezindua rasmi ofisi ya mawakala na wauzaji wao ambayo inawakutanisha wateja pamoja.
Ofisi hiyo ipo ghorofa ya tatu jengo la Faykat Tower huku ikielewezwa hatua hiyo ni muendelezo waahadi yao ya kuendelea kutoa huduma bora za bima ya Afya na bima ya Maisha kwa Watanzania.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari inaeleza Jubilee Insurance inawakaribisha mawakala na wateja wake kutembelea ofisi hizo kwa msaada zaidi kuhusu maswala ya bima.
Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wamehudhuria wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Health Insurance Dk. Harold Adamson pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jubilee Life Insurance Bi. Helena Mzena.
#Livefree



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...