Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), amezisisitiza taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya tafiti zenye tija ili kuongeza ajira kwa vijana.

Ameyasema hayo Novemba 26, 2025 alipotembelea na kuzungumza na Bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), kisha kulihakikishia Shirika hilo ushirikiano ili kuchangia kuongeza ajira kwa vijana, jambo ambalo ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Waziri Kapinga amesema ushirikiano huo utaiwezesha TIRDO kubuni vyanzo vya mapato na kufanya tafiti za kina na bunifu zitakazochochea ukuaji wa viwanda na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini, utaiwezesha TIRDO kufikia malengo yake kwa kuimarisha Uchumi kupitia kuwapa vijana ajira, kuboresha mazingira ya biashara na kuleta kiuchumi endelevu

Waziri Kapinga pia amebainisha kuwa mapato ya makaa ya mawe yaliyotokana na utafiti na uwepo wa maabara ya TIRDO yameongezeka kutoka shilingi bilioni 20 hadi kufikia bilioni 90 jambo liliookoa fedha kwa kuepuka uingizaji wa makaa ya mawe kutoka nje, kuwapa ajira vijana na wanawake na kuchagiza ukuaji wa teknolojia.

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera amelisisitiza Shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuliwezesha taifa kupata maendeleo yenye tija katika sekta ya Viwanda na Biashara.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Madundo amebainisha kuwa Shirika hilo limejipanga kuanzisha kituo maalumu cha kutengenezea vifaa vya kielektroniki kwa lengo la kupunguza utegemezi wa vifaa vya kielektroniki kutoka nje ya nchi.





























Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...