Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma.
SERIKALI imeiagiza Tume ya Madini kuwasilisha orodha ya wazalishaji wote waliopo nchini ili iweze kuwasaidia kuwakutanisha na Benki rafiki kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kujisimamia wao wenyewe.
Aidha imesema inakwenda kuimarisha kikosi kazi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi mipakani kwa ajili ya kuepusha kutorosha madini katika maeneo hayo.
Hayo yalibainishwa wa Waziri wa Madini Antony Mavunde katika ziara fupi aliyoifanya katika kiwanda cha kuyeyusha madini kilichopo Kata ya Zamahelo wilayani Bahi mkoani Dodoma.
Mavunde amesema lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kutaka malighafi za kulisha kiwanda hiko zitoke kwa wazalishaji wa hapa nchini badala ya kutoka nje ya nchi.
"Naomba hadi kufika Jumatano niwe nimepata orodha hiyo ili nami nianze mchakato wa.kuzitafuta benki hizo rafiki kwa ajili ya kuwajengea uwezo wazalishaji hao," alisema Mavunde.
Amesema Serikali inahitaji kuona wazalishaji wanaoiga hatua katika kazi wanayoifanya ndio maana wanahimiza kupata orodha ya wazalishaji wote hapa nchini.
Amesema sekta ya madini imekuwa ikichangia kiasi kikubwa cha pato la Taifa katika mfuko wa Taifa na wamejipanga kuzidisha kiwango cha uchangiaji tofauti na ilivyokuwa awali.
Hawataendelea kutumia leseni kubwa kwa mwekezaji yoyote kama hawatakuja na mpango wa kuongeza na kuendeleza thamani ya madini hapa nchini.
Akizungumzia kuhusiana na utoroshwaji wa madini,Mavunde amesema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha suala hilo halitakuwepo tena.
Mbali na hilo Mavunde amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bahi Joachim Nyingo kuhakikisha wanakisaidia kiwanda hicho ambacho ni kikubwa kati ya tisa vilivyopo Nchini wanapata kibali cha mazingira ili waweze kuanza kazi mara moja baada ya kukitembelea na kuridhishwa na maendeleo yaliyopo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Bahi Joackim Nyingo amesema kuanzia leo wanaanza kushughulikia suala hilo waliloagizwa na Waziri Mavunde ili kiwanda hiko kiweze kupata kibali na kuanza kazi mara moja kitakapokamilika.
Amesema kiwanda hicho kikikamilika.kitasaidia ajira kupatikana, lakini pia kitaongeza kukuza uchumi wa Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Dodoma na Taifa Kwa ujumla.
Kwa upande wake mwakilishi wa kiwanda hiko Hassan Ngaiza amesema ujenzi wa kiwanda hicho umekamilika kwa asilinia 80 ambapo amesema baada ya siku 40 kitakuwa kina uwezo wa kuzalisha
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Thobias Kente amesema kiwanda hicho kinakwenda kutoa ajira huku akiwataka wakazi wa Bahi kutoa ushirikiano pale wanapohitajika.
Amesema kiwanda hicho ambacho ni cha kuchenjua madini ya Nikel na Shaba kitakuwa msaada mkubwa katika maeneo mbalimbali Nchini Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...