NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijiji Homoud Jumaa ameahidi  kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)  kwa vitendo  ikiwemo kusimamia suala zima la kuwahudumia wananchi ipasavyo katika  mambo mbali mbali  kwa ajili ya kuwaletea chacu ya maendeleo katiika nyanja tofauti.

Jumaa ameyabainisha hayo wakati wa halfa fupi ya kumpokea rasmi kutokea Mkoani Dodoma ikiwa ni siku chache  zimepita baada ya kuapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini  ambapo sherehe hiyo imehudhuliwa na na viongozi wa chama cha mapinduzi, wananchama pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti.

Mbunge huyo amesema kwamba kwa sasa uchaguzi umeshamalizika na kwamba kitu kikubwa amewaomba wanachama wote na wananchi kuhakikisha kwamba wadumisha hali ya amani na utulivu wa nchi na kuepukana na vurugu ambazo hazina maana na badala yake washikamane katika kukijenga chama pamoja na kushiriki kikamilifu katika mambo ya kimaendeleo.

"Nawashukuru kwa dhati viongozi wangu wa chama cha mapinduzi, wanachama wa ccm pamoja na wananchi wote kwa kuweza kuniamini kwa mara nyingine na kuweza kunipitisha tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kitu kikubwa ambacho ninaweza kuwaahidi ni kuendelea kutoa ushirikianio wa hali na mali katika kuhakikisha  ninawaletea maendeleo mbali mbali,"amesema Jumaa.  

Katika hatua nyiingine   Mbunge huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. kwa kuweza kuchaguliwa kwa kishindo pamoja na kuweza kutoa hotuba yake nzuri ambayo imelenga kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbali mbali.

Kwa upande wake Diwani mteule wa kata ya Kwala Mansuri Kisebengo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini kwa kuweza kuchaguliwa kwa kishindo na wananchi na kwamba ana imani kubwa wataweza kuwatumikia wananchi na kuwaletea chachu ya maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata fursa ya kuhudhulia katika halfa hiyo wamesema kwamba wana imani kubwa na serikali mpya  ya awamu  ya sita  pamoja na kumpongeza Mbunge wa Jimbo hilo la Kibaha vijijini  Hamoud Jumaa kwani ataweza kuleta mafanikio ya kimaendeleo  kwa wananchi wake.

 Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijni Mhe. Hamoud Juma amepokelewa kwa kishindo kikubwa na viongozi CCM, wananchama pamoja na wananchi sambamba na madiwani  mbali mbali za Jimbo la KIbaha vijijini.                         



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...