Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Pigabet jana ilikabidhi rasmi gari jipya aina ya Toyota IST kwa mshindi wa kampeni yake ya Shinda Ndinga, David Jimloja, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa kampuni hiyo, wadau wa michezo ya kubashiri, pamoja na wananchi waliofurika kushuhudia tukio hilo ambalo limeelezwa kuwa miongoni mwa matukio yenye msisimko mkubwa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Msemaji Msaidizi wa Pigabet, Hemed Misonge, alisema kuwa ushindi wa Jimloja ni uthibitisho kwamba kampeni hiyo inalenga kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kuwapa motisha na zawadi nono.
“Pigabet itaendelea kuleta ubunifu na kampeni zenye tija kwa wateja wetu. Leo tumeshuhudia kijana wetu akitimiza ndoto ya kumiliki gari kupitia Shinda Ndinga, na bado kuna washindi wengine wengi wanakuja,” alisema Misonge.
Kwa upande wake, mshindi David Jimloja alielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa ufunguo wa gari hilo, akisema hakutarajia kama siku moja angeibuka mshindi.
“Sikuwahi kufikiria kama jina langu lingeitwa. Nawashukuru Pigabet kwa kutimiza ndoto yangu. Hii ni zawadi ambayo itabadilisha maisha yangu,” alisema kwa hisia.
Kwa upande wake, mshindi wa shindano hilo, David Jimloja kutoka Dodoma, alisema kuwa ana furaha kubwa kuona ndoto yake ya kumiliki gari ikitimia, kwani awali alikuwa akishinda fedha pekee lakini hakuwahi kukata tamaa.
“Nimekuwa nikicheza mchezo huu kila siku bila kukata tamaa. Leo ndoto yangu ya kumiliki gari yangu mwenyewe imetimia. Nawashukuru Pigabet kwa nafasi hii, na nawashauri vijana wenzangu wenye simu janja na hata zile za kawaida wajaribu bahati zao kwa uaminifu na uvumilivu,” alisema David.
Kampeni ya Shinda Ndinga imeendelea kuvutia maelfu ya washiriki nchini kote, huku Pigabet ikiahidi kuendelea kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika hatua zijazo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...