Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na Wananchi kwa ujumla kuendelea kuiombea Nchi amani na kudumisha mshikamano.
Akizungumza leo tarehe 21 Novemba 2025, mara baada ya kujumuika na Waumini katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa Masjid Rashidin, Dole Sokoni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Alhaj Dkt. Mwinyi amesema kila mwananchi ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuhimiza na kukumbusha umuhimu wa Amani nchini.
Ameeleza kuwa ni neema kubwa kuona Amani imedumu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi, jambo linalopaswa kuendelezwa kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendeleza dua na ibada.
Aidha , Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwepo kwa Amani kunaiwezesha Nchi kutekeleza kikamilifu mipango ya Maendeleo katika nyanja mbalimbali, na ameunga mkono tangazo la siku ya Jumatatu tarehe , 24 Novemba 2025 kuwa siku maalum ya Waumini kufunga na kuiombea Nchi Amani.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kwamba madhara ya kukosekana kwa Amani ni makubwa, ikiwemo kupungua kwa upatikanaji wa chakula, kupanda kwa bei za bidhaa, na kuongezeka kwa misukosuko ya kijamii, hivyo umuhimu wa kuiombea Nchi Amani haupaswi kubezwa.
Katika hatua nyingine, Alhaj Dkt. Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuwaombea dua Viongozi Wakuu wa Serikali, ili waweze kutekeleza majukumu na ahadi zao kwa uadilifu na mafanikio, akibainisha kuwa dhamana waliyopewa ni kubwa na ina hitaji msaada wa Mwenyezi Mungu.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...