Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma .

Kamishana wa Bima Tanzania Dkt  Baghayo Saqware amesema kuwa Sekta hiyo imezidi kukua sambamba na mabadiliko ya kiuchumi,kijamii na kiteknolojia na ikiwemo ongezeko la matumizi ya teknolojia ambayo imepelekea kuimarisha ushindani katika soko la Bima.

Dkt Saqware ameyasema hayo leo Jijini Dodoma November 18,2025 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Elimu ya Bima kwa Wahariri wa vyombo vya Habari Tanzania.

Ambapo amesema kuwa mpaka sasa Tanzania ina kampuni zaidi ya arobaini za Bima,mawakala,madalali na watoa huduma wengine kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa na huduma za Bima zenye ubora.

"Sekta ya bima nchini imeendelea kukua mwaka hadi mwaka sambamba na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia. Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, ongezeko la matumizi ya teknolojia, uboreshaji wa mifumo ya usajili, usimamizi wa kampuni za bima, na kuimarika kwa udhibiti kumechangia kuongeza kwa uaminifu na kuimarisha ushindani katika soko la bima".

"Tanzania kwa sasa ina kampuni zaidi ya arobaini za bima, mawakala, madalali na watoa huduma wengine wanaohakikisha wananchi wanapata bidhaa na huduma za bima zinazokidhi mahitaji yao lakini pamoja na mafanikio hayo, bado kuna changamoto kadhaa ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu na faida za bima na hapa ndipo vyombo vya habari vinapokuja kuwa kiungo muhimu".

Pamoja na hayo Dkt Saqware ametoa wito kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kuendeleeni kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Usimamaizi wa Bima (TIRA) katika kutoa elimu ya bima,Kuongeza weledi katika uandishi wa masuala ya bima na kuwa TIRA ipo tayari kushirikiana katika kutoa mafunzo na taarifa muhimu.

Kwa upande wake Bi Margareth Mngumi ambaye ni Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) amesema kuwa  ni matumaini yake kuwa mafunzo hayo yatakuwa ni mwanzo wa safari ya mabadiliko chanya na mashirikiano mazuri na yenye majadiliano ya kina ya kujenga.

 Na kuongeza kuwa Ofisi yake inatambua nguvu ya vyombo vya Habari hivyo wangependa kuanzisha ukarasa mpya wa ushirikiano ili kuboresha mazingira katika utatuzi wa migogoro ya Bima kwa Maslahi ya Watanzania. 

"TIO inatambua nguvu mlizonazo na tungependa leo tunazishe ukurasa mpya wa ushirikiano ili kuboresha zaidi mazingira ya utatuzi wa migogoro ya Bima kwa maslahi ya Watanzania".

 Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uelewa wa maswala mbalimbali yahusuyo bima,kudumisha ushirikiano baina ya TIRA na Sekta ya Habari nchini sambamba na kuongeza ubunifu katika kuelimisha Umma kuhusu masuala ya bima ili kukuza uelewa wa wananchi juu ya Soko la Bima nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...