EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KLABU ya Simba SC imeanza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Petro Atletico de Luanda ya Angola, katika mchezo wa kundi D uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Simba ilijikuta ikiruhusu bao pekee dakika ya 78, likifungwa na nyota wa Petro Atletico, Benny, baada ya kukamilisha shambulizi lililoanzia katikati ya uwanja.
Timu hiyo ya Msimbazi, ambayo ilitarajiwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani kuanza vyema kampeni zake, sasa inaburuza mkia wa kundi D ikiwa na alama sifuri.
Baada ya matokeo ya michezo ya ufunguzi, Petro Atletico wanaongoza kundi kwa pointi tatu, wakifuatiwa na Esperance de Tunisia na Stade Malien ambao wote wana pointi moja, huku Simba ikifunga orodha ikiwa na alama 0.
Simba itahitaji kufanya vizuri katika michezo yake ijayo ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...