OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), CPA. Nicodemus Mkama amesema Kampuni ya Saruji Tanga imeweka historia ya kuwa kampuni ya kwanza kwenye masoko ya mitaji ambayo imeuza hisa stahiki zenye thamani kubwa kuliko zote kuwahi kutolewa yaani shilingi bilioni 203.74 na kupata mafanikio ya asilimia 100.

CPA.Mkama ameyasema hayo leo Novemba 27,2025 wakati hafla ya kuorodheshwa kwa hisa stahiki za Kampuni ya Saruji Tanga(Tanga Cement PLC) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
“Kiasi kikubwa cha hisa stahiki kilichowahi kuuzwa katika masoko ya mitaji ni hisa stahiki zenye thamani ya shilingi bilioni 152 zilizouzwa na Benki ya CRDB mwaka 2015.
“Kuorodheshwa kwa hisa stahiki za kampuni ya Saruji Tanga hivi leo kunaongeza thamani ya mtaji wa kampuni kwa asilimia 44.82 na kufikia shilingi bilioni 658.35 kutoka shilingi bilioni 454.61.”
Aidha, amesema kuorodheshwa kwa hisa stahiki za kampuni ya Saruji Tanga kunaongeza idadi ya hisa za kampuni hii kwenye soko la hisa kwa asilimia 200 na kufikia hisa milioni 191, kutoka hisa milioni 63 huku akisisitiza hatua hiyo ina matokeo chanya katika kuongeza ukwasi kwenye soko la hisa.
.jpeg)
CPA.Mkama amesema vile vile kuorodheshwa kwa Hisa Stahiki za Kampuni ya Saruji Tanga kwenye soko la hisa, kunatoa fursa wawekezaji kuuza hisa zao pale wanapohitaji fedha kwa ajili ya matumizi mengine.
“Urodheshwaji wa hisa unawawezesha wawekezaji kujua thamani halisi ya hisa zao (Price Discovery); na kuwapatia fursa wawekezaji wapya kununua hisa hizo (trading of shares), ambapo wawekazaji wanatarajia kupata gawio kama faida itokanayo na uwekezaji huo.
“Mafanikio yaliyopatikana katika mauzo ya hisa za kampuni ya saruji Tanga ni matokeo ya mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kiutendaji yanayotolewa na Serikali kupitia CMSA).
“Ikiwa ini pamoja na CMSA kuidhinisha wanahisa wa kampuni ya Saruji Tanga kununua hisa stahiki za kampuni hii kwa bei ya shilingi 1,600 (Discounted Price), sawa na punguzo la asilimia 38.2 ikilinganishwa na bei ya soko ambayo ilikuwa ni shilingi 2,590 kipindi mauzo yalipofunguliwa.”
.jpeg)
Hivyo amesema nawapongeza wanahisa wa Kampuni ya Saruji Tanga kwa kutumia fursa hii kununua hisa stahiki za kampuni, ambazo zimewawezesha kunufaika na punguzo hili la bei; na kuimarisha uwekezaji wenu ndani ya Kampuni; na kuongeza idadi ya hisa.
Aidha amewapongeza taasisi na wadau wote waliohusika katika mchakato wa utoaji wa hisa stahiki za kampuni ya saruji Tanga. Taasisi hizo ni pamoja na Bodi na Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) waliosimamia na kutoa miongozo mbalimbali kufanikisha mchakato huo.
CPA.Mkama pia amesema Masoko ya mitaji huchochea maendeleo ya uchumi kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha na kuimarisha utawala bora na hivyo kuleta tija kwa kampuni na taasisi.
Hivyo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo.
Ameongeza ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma (equity financing); hatifungani (bonds); na vipande vya Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).




.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...