Na Emmanuel Mbatilo, Dar es Salaam
CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kimemtunuku Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Fasihi na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Mwasisi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Clementina, Dkt. Maria Josephine Kamm, kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya elimu nchini.
Dkt. Kamm ametunukiwa Digrii hiyo leo Novemba 18, 2025, wakati wa mahafali ya 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Akihutubia maelfu ya wahitimu na wageni waalikwa, Dkt. Kamm amesema kumuelimisha msichana ni hatua muhimu katika kubadili sio tu maisha ya mtu mmoja, bali pia jamii nzima kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Amehimiza jamii kutokumkatia tamaa mtoto wa kike, badala yake kuhakikisha anapata elimu bora itakayomwezesha kujikomboa na kuchangia katika ujenzi wa jamii mpya.
“Unapomuelimisha msichana, umebadilisha familia, jamii na hatimaye taifa. Elimu ni nguzo ya mageuzi ya kijamii,” amesema.
Amesema anaamini elimu inapaswa kuwa ya vitendo na inayomuandaa kijana sio tu kufaulu mitihani, bali pia kuishi maisha yenye heshima, kutatua changamoto na kuwa na manufaa katika jamii.
“Daima nimesimama kidete kuunga mkono elimu ya kujitegemea kama falsafa muhimu inayojenga kujiamini, ubunifu na ustahimilivu,” amesema Dkt. Kamm, ambaye kupitia taasisi yake amekuwa akichangia ujenzi wa miundombinu ya shule na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika elimu.
Aidha, aliwataka wahitimu kutokata tamaa pindi wanapokutana na vikwazo katika safari yao ya kujifunza na kutafuta mafanikio.
“Elimu yenu ndiyo nguvu yenu. Itumieni vyema, fanyeni kazi kwa uadilifu na lengo, na daima msisahau mlipotoka,” amewahimiza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Anangisye wakati akitoa hotuba yake, amesema zaidi ya mitaala 250 imepitiwa na inatarajiwa kuwasilishwa kwa TCU kwaajili ya kupitishwa, ambapo takribani mitaala 242 ya ngazi ya Shahada ya Awali na Uzamili tayari imewasilishwa.
"Hadi sasa, mitaala 49 imepata Ithibati kwa mwaka wa masomo 2025/2026". Amesema.
Amesema Chuo kimewezesha utambuzi wa zaidi ya bunifu 120 na usajili wa kampuni changa 39, kama sehemu ya juhudi za kukuza ubunifu na ujasiriamali.
Kuhusu Ubunifu Prof. Anangisye amesema kuwa Chuo kimetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi 569, wakiwemo wanafunzi 65 wenye ulemavu, ikiwa ni hatua ya kujenga uwezo jumuishi kwa maendeleo endelevu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...