Umoja wa mamlaka za maji nchini uholanzi (VEi) kupitia mradi wa kudhibiti Maji yanayopotea bila pato unaotekelezwa Tanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA) imeendelea na utekelezaji wa mradi wa kupambana na upotevu wa maji katika maeneo ya kihuduma sambamba na kuendeleza adhma ya kuwajengea uwezo watumishi kwa lengo la kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa kwa ufanisi na wananchi wanaendelea kuhudumiwa kwa ubora.
Katika mafunzo hayo VEi imewajengea uwezo watumishi 20 kutoka idara ya Huduma kwa wateja ambao wamepata mafunzo juu ya kupambana na maji yanayopotea Kwa lengo la kujuwa mbinu na namna ya kukabiliana na maji yanayopotea











Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...