Unaweza kusema urasi (legacy) ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika filamu ya “Tanzania: The Royal Tour” ni ngumu kufutika.

Miaka takribani minne leo tangu Rais Samia aliposhiriki kurekodi filamu hiyo kati ya Agosti na Novemba, 2021; na ikiwa ni miaka takribani mitatu tangu ilipozinduliwa mwaka 2022, viongozi waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zao leo wameienzi filamu hiyo kivitendo.

Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu wake, Mhe. Hamad Chande na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi, wamefika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na kufanya “Royal Tour.”

Pamoja na maeneo mengine viongozi hao walishiriki utalii wa kutembea kwenye daraja la kunesa la kamba lenye urefu wa jumla ya mita 450 linalopita kwa baadhi ya sehemu juu ya misitu ya hifadhi hiyo kwa urefu wa mpaka mita 18 kutoka ardhini.

Furaha ya Waziri Ashatu kushiriki utalii huo haikuishia tu hifadhini, bali ilikamilika pale aliposhuhudia makundi ya watalii wakiingia na kutoka Hifadhini hapo kuthibitisha kuwa ama kwa hakika utalii wa Tanzania uko imara na unasonga mbele.

“Hii ni nchi nzuri sana na siku zetu 12 hapa tunaona kama hazitoshi. Tutaenda na tutarudi tena,” wanasema watalii ambao ni kundi kutoka nchini Italia walipopata fursa ya kusalimiana na Waziri na viongozi wa Wizara na wale wa Tanapa.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...