NDEGE ya Shirika la Ndege Tanzania (Air Tanzania) imefanya first touch down katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Victoria Falls, Zimbabwe, leo mchana tarehe 18 Desemba 2025, hatua inayozidi kuimarisha ushirikiano wa usafiri wa anga kati ya Tanzania na Zimbabwe.

Katika safari hizo mpya, shirika hilo limetangaza ofa ya tiketi ya kurudi (return ticket) kwa USD 499, ambapo abiria wa Daraja la Biashara (Business Class) wanaruhusiwa kubeba mizigo yenye uzito wa hadi kilo 69, huku Daraja la Kawaida (Economy Class) likiruhusu mizigo ya hadi kilo 46.

Kuanzishwa kwa safari za Victoria Falls kunaifanya Air Tanzania kupanua mtandao wake wa safari nchini Zimbabwe, ambapo mji huo unakuwa kituo cha pili (second destination) baada ya Harare, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo wa kuongeza safari za kimataifa na kukuza utalii, biashara na usafiri wa kikanda.

Hatua hiyo pia inatarajiwa kuchochea zaidi sekta ya utalii, hasa kwa kuunganisha vivutio vikubwa vya utalii vya Afrika Mashariki na Kusini, ikiwemo Maporomoko ya Victoria Falls, moja ya maajabu ya dunia.








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...