Mkuu wa mkoa wa Mbeya Beno malisa ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa mbeya kuzilinda tunu za taifa za amani,umoja na mshikamano kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka za cristmas na mwaka mpya 2025.
Wito huo umetolewa December 04 mwaka 2025 katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya mbeya na Mkuu wa Mbarali Jenerali, Majid Hassan Sulumbu aliyemwakilisha mkuu wa Mbeya Mh. Beno Malisa kwenye hafla ya kukabidhi Meza 120 na Viti vyake 120 pamoja na miche ya miti 100 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa shule ya sekondari ya Ihombwe iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini kata ya Utengule Usangu vilivyotolewa na Benki ya Stanbic.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Mh. Jenerali Sulumbu amesema utolewaji wa vitu hivyo na benki ya Stanbic ni hatua muhimu katika kufanikisha jitihada za serikali kwenye maendeleo ya elimu ambapo ameipongeza benki hiyo huku akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika miundombinu ya elimu.
Awali Meneja wa Benki ya Stanbic tawi la Mbeya, Paul Mwambashi ametoa wito kwa jamii kutumia huduma za kibenki kupitia benki hiyo kwani kwa miaka 30 ya utoaji wa huduma za kifedha nchini benki hiyo imeendelea kutoa huduma bora na salama kwa watanzania.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya Ihombwe sekondari mwalimu Zackia Hassan Mwangu mara baada ya kupokea madawati hayo 120,viti 120 na miche ya miti 100 ya matunda na kivuli ameishukuru benki hiyo huku akiwataka watanzania kuiga mfano wa Stanbic katika kuboresha maendeleo ya elimu kupitia michango yao katika eneo la ziada na kiada





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...