📍 Dar es Salaam 

Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani Tume ya Ushindani (FCC) imekukutana na wadau wote wanaohusika na utoaji wa mizigo bandarini kupitia chama chao cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) ili kuwapa elimu na kuwafahamisha kuwa FCC imeingia katika mfumo rasmi wa ukaguzi bidhaa wa pamoja yaani Tanzania Other Government Agencies (TANOGA) ili kurahisisha ukaguzi wa bidhaa bandia ambapo kupitia mfumo huu ukaguzi unafanyika kwa pamoja na mamlaka zingine za udhibiti za Serikali.
Akizungumza katika semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti bidhaa Bandia wa FCC Bw. Salvatory Chuwa amesema  kuwa lengo la kuingia katika mfumo huo ambao unarahisisha shughuli za ukaguzi wa bidhaa wa kila siku ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa na mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwafanya wamiliki wa nembo za bidhaa wanapata thamani halisi ya walichowekeza sambamba na hilo ni kuhakikisha kuwa walaji wetu wanalindwa ili wawe wanapata thamani halisi ya bidhaa wanazotumia na zenye kukidhi matarajio yao.
Nae Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) Bw. Wahid Sahdin  amesema  kuwa TAFFA  itaendelea kuipa Tume ushirikiano katika kupambana na bidhaa bandia zinazoingia nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo bandari.

Tume ya Ushindani (FCC) imekuwa na kawaida ya kukutana na wadau wake mara kwa mara ikiwa ni muendelezo wa zoezi la utekelezaji wa mpango wa elimu kwa Umma unaorahisisha utekelezaji wa Sheria inazozisimamia.

Semina  hiyo ilitolewa Disemba 2, 2025 Katika ukumbi wa Mikutano wa Serengeti ulio katika ofisi za FCC, jijini Dar es Salaam.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...