NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMPUNI ya Usambazaji na Uuzaji wa Bidhaa za Haier, IBKI Enterprises Ltd, imezindua duka la kisasa la uuzaji wa bidhaa za kielektroniki katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 24, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Ibrahim Kiongozi, amesema duka hilo limeanzishwa kwa lengo la kuwapatia wananchi bidhaa bora, za kisasa na kwa bei rafiki, huku ofa mbalimbali zikiendelea kutolewa hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu.

Kiongozi amesema kuwa IBKI Enterprises ni wakala wa bidhaa za Haier kutoka nchini China na kupitia duka hilo wanalenga kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa urahisi.

“Tunazo bidhaa mpya na zenye ubora wa hali ya juu kutoka nchini China. Pia, dukani hapa kuna ofa mbalimbali tunazoendelea kuzitoa kwa wateja wetu, hivyo tunawaomba wananchi wafike kujionea na kunufaika na bidhaa zetu,” amesema Kiongozi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Haier, Liu Chi (Leon), amesema kampuni hiyo imeamua kuwekeza nchini Tanzania kutokana na mazingira mazuri ya biashara na soko kubwa la bidhaa za kielektroniki.

Leon amesema uwekezaji huo una lengo la kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata bidhaa bora, za kisasa na zinazokidhi viwango vya kimataifa.






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...